Meli tatu za kivita za Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China  zimewasili katika Bandari ya Dar es Salaam zikiwa na wanajeshi kadhaa kwa ajili ya kushiriki mazoezi ya pamoja na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ikiwa ni sehemu  maadhimisho miaka 60 ya Jeshi hilo na ushirikiano kati ya Nchi ya Tanzania na China tangu kuanzishwa kwake.

Akizungumza Julia 24, 2024 katika Bandari ya Dar es Salaam wakati akipokea Meli tatu za Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China, Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji Tanzania NAVY, Rear Admiral Ameir Ramadan Hassan, amesema kuwa  ujio wa meli hizo kutoka Jamhuri ya Watu wa China ni sehemu ya  kuadhimisha ushirikiano wa miaka 60 kati ya Tanzania na China.

Rear Admiral Ameir Ramadan Hassan amesema  kuwa wakiwa nchini  watashiriki mazoezi ya pamoja kati ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China  kwa ajili ya kudumisha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na China ambapo tangu kuanzishwa kwake imefika miaka 60.

Ad

Amesema kuwa sio mara ya kwanza Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China kuja nchini Tanzania kufanya mazoezi ya pamoja na Jeshi la JWTZ kwani mwaka 2014, 2019, 2020 walikuja kushiriki mazoezi. “Ujio wa Jeshi la Ukombozi Watu wa China tutajifunza mbinu mbalimbali kutokana  wao wameendelea zaidi katika masuala ya kijeshi” amesema. Amesema kuwa mazoezi ya pamoja na Jeshi la Watu wa China watashiriki  vikundi mbalimbali vya Jeshi la Ulinzi la Tanzania, huku akifafanua kuwa  kupitia mazoezi hayo yatawasadia kuongeza uwezo wa kijeshi katika utekelezaji wa majukumu yao.

#SisiNdioWajenziWaTanzaniaYetu #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya #MSLAC #SamiaSuluhuHassan #ChamaChaMapinduzi #PhilipMpango #wizarayaafya #wizarayaujenzi

Ad

Unaweza kuangalia pia

Askofu Dkt Maasa OleGabriel RAIS SAMIA ANATEKELEZA MAAGIZO YA MUNGU YA KUITUNZA BUSTANI YA EDENI

Askofu Dkt. Maasa OleGabriel Katibu Mkuu Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania na Askofu wa …

3 Maoni

  1. priligy generic The underlying mechanisms responsible for these alterations in water homeostasis remain to be unfolded, yet hyponatremic polydipsic schizophrenic patient display structural changes and neuroendocrine impairment affecting the anterior hippocampus which may serve as an anatomical substract for future investigations 149, 150

  2. where to buy priligy The number of phospho p38 MAPK positive parietal cells in Ink4a Arf mice after tamoxifen treatment was much higher than that in WT mice Fig

  3. com website users have most commonly reported using Tamoxifen after food can priligy cure pe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *