Maktaba ya Kila Siku: July 29, 2024

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi ametembelea kaburi la aliyekuwa Rais wa Awamu ya 3, hayati Benjamin William Mkapa katika Kijiji cha Lupaso mkoani Mtwara, Julai 28, 2024, kuhani familia na kuzungumza na wananchi wa Lupaso.

Balozi Nchimbi amesema “naomba nikiri kuwa mimi ni mwanafunzi wa hayati na nimekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa (UVCCM), katika kipindi chake. Ndiye alinilipia ada ya kusoma chuo kikuu na alikuwa mfuatiliaji sana na alitulea vizuri. Sio sisi tu, bali Watanzania wote aliwalea pia. Alikuwa mzalendo kwa nchi, alifanya …

Soma zaidi »