WANANCHI WILAYANI KILOSA WAISHUKURU SERIKALI KWA UJENZI WA DARAJA LA BEREGA

Wananchi wa Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro, wameonyesha shukrani zao kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuzindua Daraja la Berega. Uzinduzi huo ulifanyika tarehe 02 Agosti, 2024, katika ziara ya kikazi ya Rais Samia mkoani Morogoro.

Daraja hili muhimu limekuwa ni faraja kubwa kwa wananchi wa eneo hilo, kwani litaboresha kwa kiasi kikubwa usafiri na usafirishaji wa bidhaa. Wananchi wameeleza kuwa ujenzi wa daraja hili utarahisisha maisha yao kwa kuondoa changamoto za mvua na mafuriko yaliyokuwa yakitatiza mawasiliano na shughuli za kiuchumi. Aidha, wamepongeza juhudi za serikali katika kuboresha miundombinu na maendeleo kwa ujumla. Wananchi wameahidi kushirikiana na serikali katika kulinda na kuhifadhi miundombinu hiyo kwa manufaa ya wote.

Ad
Ad

Unaweza kuangalia pia

“Tukamate wajibu wetu tuliopewa na Mungu, wa Kukuza watoto wetu katika maadili mema”.‪@samiasuluhu99‬

Twende tukatunze Watoto wetu vile sisi tulivyotunzwa na Wazazi Wetu katika maadili mema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *