Wananchi Msomela Wapongeza Juhudi za Serikali, Huduma za Afya, Elimu na Maji Zawaletea Maendeleo

Wananchi wa Msomela wameonesha furaha na shukrani kwa jitihada za serikali kuhakikisha kwamba wanapata huduma muhimu kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Huduma za afya zimeimarika, huku kituo cha afya kijijini kikitoa huduma bora na za uhakika, na kuzuia magonjwa yanayoweza kuzuilika. Aidha, upatikanaji wa elimu umeboreshwa kwa kujengwa kwa shule mpya ambazo zinawawezesha watoto wa kimasai kupata elimu bila kikwazo chochote.

Wananchi pia wameelezea kuridhishwa kwao na upatikanaji wa maji safi, huduma ambayo imekuwa mkombozi mkubwa kwao, kwani awali walikuwa wakikumbana na changamoto ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji. Hivi sasa, visima na mabomba ya maji yaliyojengwa kijijini yamewapa unafuu mkubwa na kuongeza tija katika shughuli zao za kilimo na ufugaji.

Ad

#SisiNdioWajenziWaTanzaniaYetu#SSH#CCM#KaziIendelee#Nchiyangukwanza#SisiniTanzania#matokeochanya#MSLAC#SamiaSuluhuHassan#ChamaChaMapinduzi#PhilipMpango#wizarayaafya#wizarayaujenzi

Ad

Unaweza kuangalia pia

“Tusikubali Kuwa Tarumbeta za Watu Wasio Tutakia Mema”

“Tusikubali kuwa tarumbeta za Watu wasio tutakia mema, Maadili Yetu Mazuri Ya Kitanzania Lazima Tuyatunze, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *