DKT. TULIA ASISITIZA UMUHIMU WA USALAMA DUNIANI NA MAENDELEO YA PAMOJA

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa upo umuhimu mkubwa wa nchi mbalimbali hususani zile zinazounda Umoja wa G7 kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kutafuta usalama duniani na maendeleo ya pamoja na kwamba wakati umefika sasa kwa nchi hizo kushirikiana na nchi za Afrika kama washirika walio sawa. Dkt. Tulia ameyasema hayo leo tarehe 6 Septemba, 2024 wakati akishiriki Mkutano wa 22 wa Maspika wa Mabunge ya nchi za G7 unaofanyika Jijini Verona, nchini Italia ambapo alipata nafasi ya kutoa mitazamo ya IPU na Afrika juu ya masuala yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo. Mkutano huo, umehudhuriwa na Maspika kutoka Mabunge ya Italia, Ujerumani, Ufaransa, Marekani, Japan, Canada, Uingereza, Bunge la Ulaya, Ukraine na Tanzania umebeba ujumbe wa kuunganisha nchi za G7 na nchi za Afrika na Mediterania katika kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu, kuleta amani ya kudumu duniani pamoja na matumizi ya Akili Mnemba (AI) na kukabiliana na changamoto zinazotokana na matumizi hayo.

Image

Image

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *