Ujenzi wa Daraja la J.P. Magufuli (Kigongo–Busisi) umefikia hatua za mwisho. Hadi Septemba 17, 2024, ujenzi ulikuwa umefikia asilimia 90.5, na sehemu ya mita mbili pekee ilibaki ili kuunganisha daraja lote.
Daraja hili lenye urefu wa kilomita 3.2 linatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba 2024. Serikali imeendelea kutoa fedha kwa wakati, ambapo hivi karibuni zilitolewa shilingi bilioni 18 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.
Kukamilika kwa daraja hili kutarahisisha usafiri na usafirishaji kati ya mikoa ya Mwanza na Geita, na pia nchi jirani kama Uganda, Rwanda, na Burundi.