Maktaba ya Kila Siku: November 15, 2024

WAZIRI MKUU AONGOZA MAZIKO YA MAREHEMU LAWRENCE MAFURU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 15, 2024 ameungana na ndugu, jamaa, marafiki na viongozi wengine wa Serikali katika mazishi ya aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Tume ya Mipango, Marehemu Lawrence Nyasebwa Mafuru. Maziko hayo yamefanyika katika Makaburi ya Kondo, Ununio jijini Dar es Salaam. Marehemu Mafuru alifariki Novemba 09, 2024 …

Soma zaidi »

Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele katika kuhimiza ushirikishaji wa jamii katika mapambano dhidi ya njaa nchini Tanzania. Ameweka msisitizo kwenye kuboresha usalama wa chakula kupitia mipango mbalimbali inayolenga kuongeza uzalishaji wa kilimo na kuhakikisha upatikanaji wa chakula kwa wananchi wote

Katika mkutano wa G20 unaotarajiwa kufanyika Rio de Janeiro, Brazil, tarehe 18 hadi 19 Novemba 2024, Rais Samia amealikwa kushiriki kama mgeni mwalikwa. Ushiriki wake katika mkutano huu ni fursa muhimu kwa Tanzania kuwasilisha ajenda zake kuhusu usalama wa chakula na ushirikishaji wa jamii katika mapambano dhidi ya njaa. Kupitia …

Soma zaidi »

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa mkono wa pole kwa wafiwa wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Marehemu Lawrence Nyasebwa Mafuru katika Viwanja vya Karimjee

Mhe. Dkt. Kikwete alifika hapo akitokea Uwanja wa Ndege moja kwa moja akitokea kuhudhuria vikao vya Bodi ya Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia masuala ya Elimu Duniani (GPE), ambayo yeye ni Mwenyekiti wake, jijini Washington DC, Marekani.

Soma zaidi »