Hafla hiyo ilifanyika katika mkoa wa Simiyu, ambapo Waziri Mkuu alisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ipo imara na imejidhatiti kuhakikisha huduma muhimu za kijamii zinawafikia wananchi wote nchini.
Katika hotuba yake, Mheshimiwa Majaliwa aliwahakikishia wananchi kuwa Serikali itaendelea kufanya kazi kwa bidii katika kuwaletea maendeleo na kuboresha maisha yao kwa kuhakikisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji inaimarishwa ili kurahisisha shughuli za kijamii na kiuchumi.
Aidha, Waziri Mkuu alifanya ukaguzi wa ujenzi wa Daraja la Simiyu ambalo lina urefu wa mita 175, likiambatana na barabara unganishi yenye urefu wa kilomita 3. Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Mheshimiwa Majaliwa alibainisha kuwa Serikali imeamua kujenga upya daraja hilo kwa kuzingatia umuhimu wake mkubwa kwa wananchi wa mkoa wa Simiyu na maeneo ya jirani. Alisema kuwa daraja hilo lilijengwa kwa mara ya kwanza enzi za ukoloni, na sasa Serikali imeona ni vyema kulijenga upya kwa teknolojia ya kisasa ili kuboresha usalama na ustawi wa watumiaji.
“Serikali inatambua umuhimu wa daraja hili kwa maendeleo ya wananchi wa Simiyu na maeneo yanayozunguka. Lengo letu ni kuhakikisha wananchi wanaendelea kufaidika na huduma bora za miundombinu kwa ajili ya kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla,” alisema Waziri Mkuu.
Viongozi wa Serikali, wabunge, na wananchi walioshiriki kwenye hafla hizo walitoa shukrani kwa jitihada za Serikali za kuendelea kuboresha miundombinu muhimu, huku wakiahidi kushirikiana kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa viwango vya juu.
Ujenzi wa madaraja haya mawili unatarajiwa kuboresha usafiri wa watu na mizigo, kuchochea biashara, na kufungua fursa zaidi za kiuchumi kwa wananchi wa Simiyu na Tanzania kwa ujumla. #MSLAC. #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya @samia_suluhu_hassan Ikulu Mawasiliano