Makubaliano hayo yalifanyika Januari 8, 2024, jijini Dar es Salaam, yakiwa na lengo la kuongeza idadi ya watalii na wawekezaji katika sekta ya utalii nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Ephraim Mafuru, amesema wamechagua shirika hilo la ndege kutokana na kuwa na ndege zaidi ya 490 na kufanya safari zake katika miji zaidi ya 350 duniani, ikiwemo miji zaidi ya 61 barani Afrika pekee. Hivyo, Tanzania itaweza kutangazwa kikamilifu katika miji hiyo yote.
Amesema makubaliano hayo yanahusisha maeneo kadhaa, ikiwemo kutoa matangazo ya vivutio vya utalii na maeneo ya uwekezaji kwenye ndege za shirika hilo, tovuti yao, na ofisi zao duniani kote. Pia, abiria, hususani wa Tanzania, watanufaika na punguzo la nauli kwa safari zinazolenga kutangaza utalii wa Tanzania. Aidha, Mafuru ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa juhudi zake za kufungua nchi katika sekta ya utalii duniani.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Uturuki nchini Tanzania, Kadir Karaman, amesema makubaliano hayo yataimarisha lengo la pamoja la kuifungua Tanzania kwa masoko ya kimataifa ya utalii, na kuleta ukuaji wa sekta hiyo kwa manufaa ya pande zote mbili.\
Ameongeza kuwa kuanzia Juni, shirika hilo litaongeza safari zake nchini Tanzania, ambapo safari za kwenda Kilimanjaro zitaongezeka kutoka 4 hadi 14 kwa wiki, na safari za kwenda Zanzibar kutoka 9 hadi 14 kwa wiki. #MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya @samia_suluhu_hassan Ikulu Tanzania