Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ) Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi hiyo uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Januari, 2025

Katika Mkutano huo, Mhe. Rais Dkt. Samia alishiriki pamoja na Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema sambamba na Rais wa Jamhuri ya Malawi Mhe. Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera. Aidha, Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antoine Tshisekedi walishiriki kwa njia ya mtandao.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Taifa Bw. Murshid Hashim Ngeze mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 39 wa ALAT uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *