Ushiriki wa Tanzania katika Utayarishaji wa Filamu ya Kimataifa

Mafanikio ya Mufasa: The Lion King yamepata uzito mkubwa kutokana na mchango wa wataalamu wa Tanzania. Mtayarishaji maarufu Mussa Ally Mbwego (Mussa Kaka) ameongeza umaarufu wa nchi yetu kupitia utumiaji wa teknolojia ya kisasa katika utayarishaji wa filamu. “Ni heshima kubwa kwangu kuwakilisha Tanzania katika mradi huu wa kimataifa, ambapo tunahakikisha kuwa mandhari ya kipekee ya nchi yetu yanawasilishwa kwa uzuri wake wa asili,” alisema Mbwego alipokuwa akishiriki katika majadiliano.

Mkutano wa Bodi ya Filamu Tanzania uliofanyika tarehe 31 Januari, 2025 ulileta mazungumzo ya kina kuhusu ushiriki wa Tanzania katika filamu hizi za kigeni. Majadiliano hayo yalihudhuriwa na viongozi wa sekta ya filamu, wakiwemo:

Ad

Dkt. Gervas Kasiga (Chuma), Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu. Emmanuel Ndumukwa, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Filamu. Benson Mkenda, Afisa Mwandamizi wa Filamu Maendeleo.

Katika mjadala huo, wakurugenzi wa filamu wa ndani walitambua umuhimu wa kulinda mazingira na tunu za taifa. Walisisitiza kuwa ushiriki wa wataalamu wa ndani sio tu kwamba unakuza utamaduni wa filamu ya Tanzania bali pia unaleta fursa nyingi zaidi za kipato na ujuzi kwa watayarishaji wa ndani.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Taifa Bw. Murshid Hashim Ngeze mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 39 wa ALAT uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *