GAIRO: Gairo yafaidika milioni 135 katika Elimu

Mkuu wa wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchemba akiongozana na DED na Meneja TARURA wamefanya ziara Kata ya Mandege vijiji vya Njungwa na Ikwamba.

Mbali na barabara kuwa changamoto wamefanikiwa kufika katika kata hizo. Katika kuboresha miundo mbinu ya barabara tayari TARURA wameanza ujenzi wa barabara hizo.

Ad

Wananchi wa Gairo wametoa shukrani kwa Rais Mhe. Dr. John Pombe Magufuli kwa kuwapatia Milioni 135 ambazo zimetumika kujenga madarasa ya kisasa, nyumba za waalimu na vyoo vya kisasa Njungwa na Nongwe Sekondari.

Mkuu wa Wilaya Mhe. Siriel Shaidi Mchembe baada ya ukaguzi na kupokea taarifa ya miradi amempongeza Mkurugenzi Bi. Agnes Mkandya kwa kazi nzuri ya usimamizi wa miradi hiyo. “Kwa kweli jambo hili linapendeza machoni pa Mungu na wanadamu pia”. Alisema Mhe. Mchembe.

Wananchi wameongeza kusema kwamba Mandege na Nongwe ya miaka mitatu.iliyopita sio ya leo. Miaka mitatu ya Magufuli imefanya maajabu Tarafa ya Nongwe Gairo.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mama Mzazi wa Mama Janeth Magufuli (Juliana Stephano Kidaso) katika eneo la Kigongo Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *