RAIS MSTAAFU JK AONGOZA KIKAO CHA KAZI NA SHIRIKISHO ZA KIUCHUMI AFRIKA

  • Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika nafasi yake ya mjumbe wa taasisi ya kutokomeza malaria (End Malaria Council) jana aliendesha kikao cha kikazi na wakuu mbalimbali wa Shirikisho za Kikanda za Kiuchumi za Africa. Katika Kikao hicho Mhe. Kikwete alielezea umuhimu wa kuwekeza nguvu za pamoja katika kuutokomeza ugonjwa wa malaria katika bara letu la Afrika. Katika Mwaka 2017.
JAKAYA KIKWETE
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na Katibu Mkuu wa SADC Dr. Stergomena Tax, katika kikao cha kikazi na wakuu mbalimbali wa Shirikisho za Kikanda za Kiuchumi za Afrika.
  • Malaria iliua watu 435,000 duniani, wengi wao wakiwa ni watoto. Asilimia tisini ya vifo hivyo vilitokea Africa. Pamoja na kuwa kumekuwa na juhudi kubwa za kutokomeza malaria, Ugonjwa huo umeendelea kuwa tishio kubwa katika juhudi za maendeleo. Ni katika kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo, Mhe. Kikwete na taasisi ya kutokomeza malaria imeonelea ishirikiane na shirikisho hizo za kikanda kuwa na mikakati ya pamoja katika kutokomeza malaria.
JAKAYA
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na Katibu Mkuu wa SADC Dr. Stergomena Tax, pamoja na wajumbe wengine walioshiriki katika kikao cha kikazi na wakuu mbalimbali wa Shirikisho za Kikanda za Kiuchumi za Afrika
  • Mhe. Kikwete aliitambulisha rasmi taasisi hiyo ya kutokomeza malaria kwa wajumbe,Taasisi hiyo iliyoanzishwa na Bill Gates pamoja na Ray Chambers kwa kushirikiana na taasisi ya wadau wa malaria inayojulikana kama Roll Back Malaria Partnership to end Malaria inajumuisha viongozi wenye nguvu za ushawishi na pia watu wenye uwezo wa kifedha ambao huziwekesha kwenye shughuli za maendeleo. Wajumbe kwenye taasisi hiyo ni Bill Gates, Ray Chambers .Peter Chernin, Aliko Dangote, Mhe.Jakaya Kikwete, Graça Machel, Luis Alberto Moreno, Mhe. Ellen Johnson Sirleaf, na mwenyekiti wa ALMA ambaye kwa kipindi hiki ni Mfalme Mswati III wa Ufalme wa Eswatini.
JAKAYA
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akiongea katika kikao cha kikazi na wakuu mbalimbali wa Shirikisho za Kikanda za Kiuchumi za Afrika
  • Ikumbukwe kuwa Mhe. Kikwete ni mkereketwa mkubwa katika masuala ya Afya,na katika kipindi chake cha urais aliweza kushirikisha maraisi wa Afrika kupambana na malaria kupitia chombo alichokianzisha kinachojulikana kama African Leaders Malaria Alliance (ALMA).
  • Katika kikao hicho Katibu Mkuu wa secretariat ya chombo hicho alimshukuru Mhe. Kikwete kwa kuanzisha chombo hicho ambacho kilianza na marais nane na sasa kinajumuisha marais wote wa Africa.
  • Naye Katibu Mkuu wa SADC Dr. Stergomena Tax, alisema taasisi yake ipo tayari kufanya kazi na Mhe. Kikwete na taasisi ya kutokomeza malaria, kwani kwa SADC suala la malaria limepewa kipaumbele kikubwa. Wajumbe wote waliokuwapo katika kikao hicho wakiwemo wawakilishi wa umoja wa Afrika na RBM walimpongeza mhe. Kikwete kwa uongozi wake katika masuala ya malaria na kuelezea utayari wao wa kufanya kazi pamoja naye na na taasisi ya kutokomeza malaria.
Ad

Unaweza kuangalia pia

TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE(JKCI) KUJENGA HOSPITALI KUBWA YA MOYO MLOGANZILA

Serikali kupitia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) ikishirikiana na Serikali ya China wanatarajia kujenga …

Oni moja

  1. hongera sana Mh.J.K kuendelea kutupa heshima kimataifa.
    Mchango wako unapo thaminiwa inamaana na Taifa lako linathaminiwa pia
    Mungu atupe vijana wengi zaidi nafasi ya kwenda kimataifa na kuweza kupaisha taifa letu.
    Hongera pia kwa Rais wetu JPM kuendelea kutupaisha kwa miundo mbinu kwa mwendo wa Jet

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *