- Vijana wa kijiji cha Chihwindi kata ya Mtumachi, Newala mkoani Mtwara wamefyeka uwanja wa kijiji hicho kwaajili ya ujenzi wa kiwanja hicho cha timu ya kijiji maarufu kwa jina la POCHI NENE.
- Akizungumzia tukio hilo Ndugu Musa Shaibu, amesema kuwa wamefanya hivyo kwa lengo la kuhamasisha vijana kujitolea kufanya kazi ambazo zipo ndani ya uwezo wao badala ya kusubiri kufanyiwa kazi na Serikali
- “Tumeamua kufanya kazi hii ya kufyeka uwanja huu ili kuisadia timu ya kijiji chetu kupata uwanja wa kufanyia mazoezi kwa lengo la kukuza michezo kwani kuna vijana wengi wenye uwezo mkubwa katika michezo lakini wanakosa sehemu za kufanyia mazoezi”amesema Musa
- Aidha amesema kuwa watafanya harambee ya kutafuta fedha kwa ajili ya kununua vifaa mbali mbali vya michezo vinavyohitajika kwa ajili ya timu ya kijiji hicho,ameongeza kuwa wameafanya hivyo ili vijana wajipatie ajira kupitia michezo kwani michezo ni moja ya sekta ambayo inatoa ajira kwa vijana.
Ad