Matokeo ChanyA+

Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu EWURA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Bw. Felix Ngamlagosi. Bw. Felix Ngamlagosi amesimamishwa kazi kuanzia leo tarehe 11 Juni, 2017. Gerson Msigwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU Dar …

Soma zaidi »

Kamati ya Pili ya Mchanga wa Madini kuwasilisha ripoti yake kwa Rais Magufuli Jumatatu 12 Juni, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli atapokea taarifa ya kamati ya pili ya wachumi na wanasheria iliyofanya uchunguzi madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga wa madini yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini Jumatatu tarehe 12 Juni, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Tukio hili …

Soma zaidi »

Balozi wa China Dkt. Lu Youqing ampongeza Rais Magufuli na Serikali yake kwa bajeti nzuri

Balozi wa China hapa nchini Mhe. Dkt. Lu Youqing amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake, kwa bajeti nzuri iliyowasilishwa jana tarehe 08 Juni, 2017 Bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango. Mhe. Dkt. Lu Youqing …

Soma zaidi »

Rais Magufuli amuapisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bibi Anna Elisha Mghwira Ikulu Dsm

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Juni, 2017 amemuapisha Bibi Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Bibi Anna Elisha Mghwira amejaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Saidi Meck Sadiki aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo. Hafla ya kuapishwa kwa …

Soma zaidi »

Rais Magufuli aishukuru Kuwait kwa kutoa Bilioni 110 za barabara ya Nyahua – Chaya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameishukuru Serikali ya Kuwait kwa kutoa mkopo wa Dola za Marekani Milioni 51 sawa na takribani Shilingi Bilioni 110 kwa ajili ya kujenga barabara ya Chaya – Nyahua Mkoani Tabora yenye urefu wa kilometa 85 ambayo itaunganisha mawasiliano …

Soma zaidi »

Rais Magufuli awataka Watanzania kupuuza mjadala wa kuongeza kipindi cha Urais

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 13 Januari, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Baada ya mazungumzo hayo …

Soma zaidi »