Makamu wa Rais

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Sekretariet ya Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) wakiongozwa na Mkurugenzi wa Masuala ya Ushirikiano katika Usimamizi na Menejimenti ya Taka za Plastiki Bi. Clemence Schmid, Chamwino Dodoma

Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais amesema serikali imedhamiria kushirikiana na wadau, sekta binafsi pamoja na jumuiya ya kimataifa katika kupambana na tatizo la taka za plastiki nchini. Amesema uzoefu unaonesha kwamba ushirikiano ni njia bora zaidi itakayowezesha kukabiliana na tatizo hilo kwani yapo maeneo ambayo taka za plastiki hutupwa …

Soma zaidi »

“Amani Iliyopo Tanzania Itumike Kuleta Soko la Madini Afrika Nchini Tanzania, kwa Uchumi Imara”.

“Wachimbaji wadogo wanafanya shughuli za uchimbaji kwa kubahatisha na matokeo yake wanatumia muda mwingi na nguvu kubwa na kuambulia kidogo tu kwa hiyo Wizara ya madini inabidi iongeze wigo katika namna bora ya uchimbaji wa madini.” Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Soma zaidi »

“Uchafuzi wa mazingira katika Majiji, Miji na Halmashauri bado ni tatizo”

Makamu wa Rais ametoa maagizo wakati akifungua Kongamano la Wadau wa Mazingira lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Dar es Salaam. Amesema uchafuzi wa mazingira katika Majiji, Miji na Halmashauri bado ni tatizo huku uharibifu wa misitu ukiendelea kuwa changamoto licha ya kuwepo kwa vyombo vya …

Soma zaidi »

Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwapungia mkono Wafanyakazi mbalimbali waliojitokeza katika Sherehe za Mei Mosi wakati akiwasili katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani tarehe 01 Mei 2024.

Soma zaidi »

Je, mikakati hii ya uongozi wa Dkt. Mpango inaweza kuwa dira ya mafanikio ya maendeleo ya taifa letu?

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango, ameonyesha falsafa ya uongozi inayojikita katika maadili, utendaji wenye tija, na maendeleo ya taifa. Maadili na Uwajibikaji: Dkt. Philip Mpango anasisitiza maadili na uwajibikaji katika uongozi wake. Anaamini katika uadilifu, uwazi, na kufuata misingi ya utawala bora katika …

Soma zaidi »