Waziri Mkuu

WAZIRI MKUU MAJALIWA: MAWAZIRI SIMAMIENI UJENZI WA OFISI ZENU MJI WA SERIKALI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza Mawaziri na Makatibu Wakuu wasimamie kikamilifu awamu ya pili ya mpango wa ujenzi wa Mji wa Serikali ulipo Mtumba jijini Dodoma ili ukamilike kwa wakati. Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Septemba 8, 2021) wakati akiongoza Kikao Kazi cha Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Katibu Wakuu …

Soma zaidi »

WAZIRI MKUU MAJALIWA: MARA WEKENI MKAKATI WA KUITANGAZA MBUGA YA SERENGETI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa Mkoa wa Mara na Watendaji katika Sekta ya Utalii wabadilike na waweke mkakati wa kuitangaza mbuga ya Serengeti ili kuweza kuvutia zaidi watalii na kuitambulisha mbuga hiyo kuwa iko mkoa humo. Amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan …

Soma zaidi »

MAJALIWA AAGIZA UCHUNGUZI WATENDAJI WIZARA YA FEDHA

Waziri Mkuu, Mheshimwa Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Mkaguzi Mkuu,  Mkaguzi  Msaidizi pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha  za umma zinazowakabili. Akizungumza katika Kikao Kazi na Waziri wa Fedha na Mipango, Kaibu Mkuu,Manaibu  Katibu Wakuu na Watendaji Waandamizi wa Wizara …

Soma zaidi »

MAJALIWA – WATENDAJI SEKTA YA MAJI FANYENI KAZI WA UZALENDO

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka viongozi na watendaji wote wa sekta ya maji nchini kufanya kazi kwa uzalendo, bidii na weledi na kwa kutanguliza maslahi mapana ya nchi. Amesema lengo ni kuhakikisha kuwa kiwango cha upatikanaji wa huduma ya maji nchini kinaongezeka ili kufikia malengo ya kufikisha maji kwa kiwango cha …

Soma zaidi »

WAZIRI MHAGAMA ATOA WIKI MBILI CHANGAMOTO MRADI WA MKULAZI KUTATULIWA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama ameiagiza kamati elekezi ya Kusimamia Mradi wa Mkulazi Estate, kuhakikisha ndani ya wiki mbili ujenzi wa barabara na uwekaji umeme kwenye eneo la mradi huo, ili kuruhusu shughuli za utekelezaji wa mradi …

Soma zaidi »

WAZIRI MKUU MAJALIWA: RC NJOMBE FUATILIA MADAI YA WAKULIMA WA CHAI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhandisi Marwa Mwita Rubirya afuatilie na kuchukua hatua kwa baadhi ya viwanda vya chai vinavyonunua majani mabichi ya chai ambavyo vimekuwa vikichelewesha malipo ya wakulima ahakikishe vinawalipa kwa wakati. Pia, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Kilimo ianzishe minada ya kuuza …

Soma zaidi »

WAZIRI MKUU MAJALIWA: RAIS MAGUFULI AMEDHAMIRIA KUBORESHA MIUNDOMBINU NCHINI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameamua kuboresha miundombinu mbalimbali ya usafiri nchini ikiwemo ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa (SGR) ili kurahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo. Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Machi 5, 2021) baada ya kukagua maendeleo ya sehemu ya kipande cha pili …

Soma zaidi »

NAIBU WAZIRI KATAMBI AHIMIZA WAGENI WALIOAJIRIWA NCHINI KURITHISHA UJUZI KWA WAZAWA

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi amewataka wageni walioajiriwa nchini kwenye miradi mbalimbali ikiwemo ya kimkakati kuhakikisha wanatekeleza mpango wa urithishaji ujuzi “Succession Plan” kwa wafanyakazi wazawa kama inavyoelekezwa kwenye Sheria ya kuratibu Ajira kwa Wageni. Hayo yameelezwa Mkoani Mara, …

Soma zaidi »

WAZIRI MKUU MAJALIWA: TPA IMARISHENI USIMAMIZI WA ‘FLOW METER’

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ihakikishe inaendelea kuimarisha usimamizi wa mitambo ya mita za upimaji wa mafuta (Flow Meter) ili kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali. Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali inataka kuona makusanyo yote ya mapato kutoka katika bandari zote nchini yanayokusanywa na TPA …

Soma zaidi »

WAZIRI MHAGAMA ATATUA KERO ZA WAFANYAKAZI KATIKA SHAMBA LA MKONGE LA KIGOMBE ESTATE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ametatua kero na changamoto zilizokuwa zikiwakabili wafanyakazi wa Shamba la Mkonge la Kigombe Estate, Wilayani Muheza dhidi ya mwajiri wao kufuatia malalamiko ambayo yaliwasilishwa wakati wa ziara ya Waziri …

Soma zaidi »