WIZARA YA KILIMO

WALIOKAIDI MKATABA WA NARCO KIKAANGONI NDANI YA SIKU KUMI

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki ametoa siku kumi kwa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kubaini na kuwanyang’anya maeneo, wawekezaji waliopatiwa vitalu katika ranchi za taifa ambao wamebadili matumizi ya ardhi kinyume na makubaliano ya mikataba yao. Waziri Ndaki amebainisha hayo jana (12.01.2021) wakati alipotembelea Ranchi ya …

Soma zaidi »

HALMASHAURI ZAONYWA WAFANYABIASHARA KUCHANJA MIFUGO, MIKATABA YAO KUVUNJWA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki amepiga marufuku halmashauri zote nchini kutotumia wafanyabiashara kuchanja mifugo na kutaka kuvunjwa kwa mikataba hiyo mara moja. Waziri Ndaki amebainisha hayo jana (31.12.2020) alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Shinyanga ambapo alipokuwa katika josho la kuogeshea mifugo la Kijiji cha …

Soma zaidi »

TARI NALIENDELEA KUONGEZA UZALISHAJI WA ZAO LA KOROSHO MKOANI RUKWA

Bodi ya Korosho Tanzania kwa ushirikiano na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kituo cha Naliendele Mkoani Mtwara Imemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo kilo 400 za mbegu za korosho ili aweze kuzigawa kwa Wakuu wa Wilaya na hatimae kuwafikia wakulima kupitia Maafisa kilimo wa halmashauri …

Soma zaidi »

WAZIRI MKUU APIGA MARUFUKU TOZO YA UNYAUFU, AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI MKURURGENZI MKUU BODI YA MAGHALA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza Waendesha Maghala kuacha kukata tozo ya unyaufu kwenye zao la korosho kwa wakulima na wanunuzi kwa kuwa tozo hiyo imeshaondolewa na suala la unyaufu halijthibitishwa kitaalamu. Ametoa agizo hilo Jumamosi (Novemba 18,2020) wakati wa kikao kati yake na Wakuu wa Mikoa ya Pwani, Lindi , …

Soma zaidi »

BODI YA USHAURI NFRA YARIDHISHWA NA UJENZI WA MAGHALA NA VIHENGE VYA KISASA

Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula-NFRA wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri Mhandisi Eustance kukagua hatua zilizofikiwa za ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa katika eneo la Maisaka Mjini Babati katika Mkoa wa Manyara, tarehe 25 Novemba 2020.  Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Taifa wa …

Soma zaidi »

KATIBU MKUU KUSAYA AFUNGUA MAONESHO YA SIKU TATU YA KILIMO MSETO MKOANI MARA

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Malima (kushoto) akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya (kulia) jana mara baada ya mazungumzo yao Ofisini kwa Mkuu huyo wa Mkoa mjini Musoma. Serikali imezitaka taasisi na mashirika binafsi yanayopokea fedha toka kwa wahisani na wafadhili hususan kutoka nje …

Soma zaidi »

KATIBU MKUU KUSAYA AKARIBISHA WAWEKEZAJI KUZALISHA MBEGU ZA MAZAO YA KILIMO

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya akitazama mti bora wa kahawa katika shamba la kituo cha utafiti TACRI Mbimba wilaya ya Mbozi jana. Kushoto ni Mtafiti Mkufunzi Dismas Pangaras na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Uendelezaji Mazao Wizara ya Kilimo Beatus Malema. Wizara ya Kilimo imetoa wito kwa wawekezaji …

Soma zaidi »

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA PROGRAMU YA UGAWAJI WA MBOLEA KWA WAKULIMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Kilimo ihakikishe mbolea iliyotolewa bure kwa wakulima wadogo inawafikia na kuwanufaisha wahusika kama lengo la kampuni ya YARA lilivyokusudia. Akizungumza wakati alipozindua rasmi mpango wa ugawaji wa mbolea bure kwa wakulima katika Ofisi za Kampuni ya YARA Tanzania jijini Dar es salaam (Jumapili, …

Soma zaidi »

WAZIRI MKUU ATOA SIKU TATU KWA WIZARA YA KILIMO

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa siku tatu kwa Wizara ya Kilimo kukutana na menejenti ya kampuni ya utengenezaji na usambazaji wa mbolea ya YARA ili kuhakiki na kupata ithibati ya mbolea ya bure itakayogawiwa kwa wakulima wadogo nchini kupitia mpango wa Action Africa. Ametoa wito huo (Jumatano, Oktoba 7, 2020) …

Soma zaidi »

KILIMO CHA UMWAGILIAJI KIMEONGEZA UZALISHAJI WA MPUNGA TOKA WASTANI WA TANI 4.0 MWAKA 2014 HADI TANI 7.2 KWA MWAKA 2019

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya amewaeleza wahandisi wa umwagiliaji mikoa kuwa wana deni la kurejesha imani kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutekeleza miradi yenye ubora na tija ya uzalishaji mazao ya wakulima kwa kuwa fedha nyingi za umma zinatumika. Katibu Mkuu amesema hayo mkoani Morogoro …

Soma zaidi »