WIZARA YA MADINI

SOKO LA DHAHABU MKOANI GEITA LACHANGIA MAPATO YA SERIKALI KUPITIA MRABAHA NA ADA YA UKAGUZI KWA JUMLA YA BILIONI 36.57

Na Nuru Mwasampeta, WM WAZIRI wa Madini, Doto Biteko amewataka Watanzania kuutazama mchango wa sekta ya madini kwa namna unavyosaidia kuinua sekta nyingine za uchumi, kwani tayari kwa upande wa kuongezeka kwa ukusanyaji wa maduhuli sekta hiyo imeonesha mafanikio makubwa. “Niliwaambia wenzangu wizarani, lazima tuhame sasa kwenye mfumo wa kufurahia …

Soma zaidi »

RAIS MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama kwa dakika moja pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mawaziri pamoja na Manaibu Mawaziri ili kumkumbuka na kumuombea aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Marehemu Balozi Augustine Mahiga …

Soma zaidi »

KAMPUNI YA BARRICK YAILIPA SERIKALI DOLA MILIONI 100

Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) wa pili kushoto, akipokea hundi kifani ya dola milioni 100 kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Kampuni ya Barrick Bw. Hilaire Diarra (wa pili kushoto), Jijini Dodoma Tarehe 26 Mei, 2020, ikiwa ni sehemu ya malipo ya dola milioni 300 …

Soma zaidi »

SERIKALI YAWATAKA MAAFISA MADINI KUTHIBITISHA USHURU MIGODINI

Waziri wa Madini Doto Biteko akikagua shughuli za uchimbaji madini katika eneo la Lusu, wilayani Nzenga Mkoa wa Tabora. Serikali imesema Ushuru wowote unaotolewa kwenye Maeneo ya Migodi Nchini ni lazima uthibitishwe na Maafisa Madini walioko kwenye maeneo husika. Tamko hilo lilitolewa Mei 24, 2020  na Waziri wa Madini Doto Biteko …

Soma zaidi »

WAZIRI BITEKO: MAKUSANYO SEKTA MADINI YAONGEZEKA KUTOKA BILIONI 39/- HADI BILIONI 58/- KWA MWEZI APRILI

Nuru Mwasampeta na Tito Mselem, Dodoma Waziri wa Madini, Doto Biteko amesema ukuaji wa Sekta ya Madini unakua kwa kasi na kuifanya kuwa sekta ya kwanza kwa ukuaji kwa mwaka 2019 ikifuatiwa na sekta ya ujenzi. Ukuaji wa Sekta ya Madini umeongezeka na kufikia asilimia 17.7 kutoka ukuaji wa asilimia …

Soma zaidi »

NAIBU WAZIRI NYONGO AUTAKA UONGOZI WA STAMIGOLD KUSHIRIKIANA NA WAFANYAKAZI KUZALISHA KWA UFANISI

Meneja wa uchimbaji, Mhandisi Benson Mgimba akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Madini na walioambatana naye wakati wa ziara ya kikazi mgodini hapo. (Picha na Wizara ya Madini). Na Nuru Mwasampeta, WM Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ameutaka uongozi wa Mgodi wa Stamigold kuwajali wafanyakazi na kufanya kazi kwa …

Soma zaidi »

NAIBU WAZIRI NYONGO AWATAKA VIONGOZI WA VIJIJI KUSHIRIKI KUTOA ELIMU YA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MADINI KUPUNGUZA MIGOGORO

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ameutaka uongozi wa Kijiji cha Buhunda maarufu kama Lushokela kilichocho wilayani Misungwi mkoani Mwanza kutoa elimu ya uwekezaji kwa wananchi wake ili kuwa na uelewa juu ya masuala ya uwekezaji katika sekta ya madini. Naibu Waziri Nyongo alitoa maelekezo hayo Aprili 12, 2020 alipotembelea …

Soma zaidi »

UJENZI KIWANDA CHA KUCHAKATA DHAHABU WASHIKA KASI MKOANI MWANZA

Mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata madini ya dhahabu nchini umeshika kasi huku ujenzi wake ukitarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Septemba 2020 na kuifanya dhahabu ya Tanzania kusafirishwa ikiwa tayari imechakatwa na hivyo kuongeza thamani ya madini hayo katika soko la dunia.Ujenzi wa kiwanda hicho ulianza rasmi mwezi Machi, 2020 …

Soma zaidi »