Zuena Msuya na Henry Kilasa, Pwani Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani amewaeleza watanzania kuwa mradi wa kufua Umeme wa Julius Nyerere ( JNHPP) utaanza kuzalisha Umeme utakaotumika katika gridi ya taifa kuanzia Mwezi Juni 2022 kwa kuwa hatua ya ujenzi ya maeneo muhimu ya kuzalisha umeme yamefikia 52.8% mpaka sasa. …
Soma zaidi »ZAIDI YA BILIONI 7 ZATUMIKA KUFIKISHA UMEME KISIWA KILICHOPO ZIWA TANGANYIKA
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kupitia Nakuroi Investment Co. Ltd inayotekeleza Mradi wa awamu ya tatu mzunguko wa kwanza wanaendelea na zoezi la kulaza nyaya chini ya maji katika ziwa Tanganyika ili kufikisha umeme katika kisiwa cha Mandakerenge, kilichopo kata ya Kipili Wilayani Nkasi, Mkoani Rukwa. Zoezi hilo litakalogharimu zaidi …
Soma zaidi »SERIKALI INAHITAJI SHILINGI TRILIONI NANE KUSAMBAZA UMEME KATIKA VITONGOJI VYOTE
Na Jaina Msuya – REA Serikali inahitaji zaidi ya Shilingi Trilioni Nane kwa ajili ya kusambaza miundombinu ya umeme katika vitongoji ambavyo havijafikiwa na nishati hiyo. Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo alisema hayo katika Mkutano wa Kwanza wa Mwaka kati ya Wakala wa Nishati Vijijini …
Soma zaidi »KITUO KIPYA CHA UMEME MTERA KIKAMILIKE KABLA YA OKTOBA – NAIBU WAZIRI BYABATO
Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato ameagiza kuwa, ujenzi wa kituo kipya cha kupoza umeme cha kV 220/33 katika Kituo cha umeme cha Mtera ukamilike kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu. Alitoa agizo hilo tarehe 9 Mei,2021 wakati alipofanya ziara katika kituo cha kufua cha umeme cha Mtera na …
Soma zaidi »WAZIRI WA NISHATI APONGEZA WAFANYAKAZI KWA KUCHANGIA UCHUMI WA KATI
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani amewapongeza wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa kufanya kazi kwa ufanisi ambao umechagiza nchi kuingia katika uchumi wa kati kutokana na uwepo wa nishati inayotabirika. Dkt.Kalemani ametoa pongezi hizo jijini Dodoma, tarehe 5 Mei, 2021 wakati akifungua Mkutano Maalum wa Baraza la …
Soma zaidi »MAJALIWA: SERIKALI ITAENDELEA KUTOA FEDHA ILI KUKAMILISHA MRADI WA UMEME WA MAJI MTO RUFIJI
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewahakikishia Watanzania kwamba Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan itaendelea kutoa fedha za kugharamia mradi wa kufua umeme kwa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) ili ukamilike kwa wakati. Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Aprili 10, 2021) baada ya kukagua mwenendo wa mradi huo, …
Soma zaidi »KATIBU MKUU NA NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA NISHATI WAANZA KAZI RASMI
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja na Naibu Katibu Mkuu, Kheri Abdul Mahimbali wakiwa katika mazungumzo mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara ya Nishati, Mtumba jijini Dodoma. Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja na Naibu Katibu Mkuu, Kheri Abdul Mahimbali, tarehe 8 …
Soma zaidi »DKT. KALEMANI AZINDUA MATUMIZI YA GESI ASILIA KATIKA MAGARI YA DANGOTE
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amezindua matumizi ya Gesi asilia katika magari (CNG) ya kampuni ya kiwanda cha kutengeneza Saruji cha Dangote katika kufanya safari zake badala ya kutumia mafuta. Dkt. Kalemani alifanya uzinduzi huo wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Mtwara ya kutembelea Kiwanda cha Dangote, kukagua …
Soma zaidi »WAZIRI WA NISHATI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA KITUO CHA KUPOZA UMEME SIMIYU
Na Zuena Msuya, Simiyu Waziri wa Nishat, Dokta Medard Kalemani ameweka jiwe la msingi na kuzindua Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Imalilo kilichopo wilayani Bariadi mkoani Simiyu. Akizungumza wakati wa akiweka jiwe la Msingi, Machi 3, 2021,Dkt. Kalemani amesema kuwa Ujenzi wa kituo hicho utakamilika ndani ya kipindi …
Soma zaidi »MATENGENEZO YA MITAMBO YA UMEME NCHI NZIMA YAKAMILIKE NDANI YA SIKU TANO – DKT. KALEMANI
Na Teresia Mhagama, Dar es Salaam Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani ameagiza kuwa, matengenezo ya mitambo mbalimbali ya kufua umeme nchini yakamilike ndani ya siku Tano ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata umeme wa uhakika. Dkt. Kalemani ametoa agizo hilo tarehe 2 Machi, 2021 mkoani Dar es Salaam, mbele ya Bodi …
Soma zaidi »