Recent Posts

SERIKALI YAKUSANYA KODI YA SH.BILLION 5.5 ZA TAULO ZA KIKE

Sserikali imesema kuwa katika mwaka wa fedha 2016/17 hadi 2017/18 ilikusanya kodi ya ongezeko la thamani(VAT) ya kiasi cha Sh. Bilioni 5.5 kwenye bidhaa ya taulo za kike ‘Sanitary Pads’ zilizoingizwa nchini kabla ya kodi hiyo kuondolewa Juni mwaka jana. Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa Fedha …

Soma zaidi »

WAZIRI MKUU ATEMBELEA OFISI MPYA ZA WIZARA YA NISHATI, MTUMBA, DODOMA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amefanya ziara ya kukagua ofisi mpya za Wizara ya Nishati na Wizara nyingine zilizopo Mtumba jijini Dodoma ili kuona kama lengo la Serikali la kutoa huduma kwa wananchi katika eneo hilo limefanikiwa. Waziri Mkuu alifanya ziara hiyo tarehe 23 Aprili, …

Soma zaidi »

WAGONJWA 15 KUPATA MATIBABU YA KUZIBUA MISHIPA YA DAMU YA MOYO

Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na mwenzao wa  Hospitali ya Meditrina ya nchini India wanafanya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa  siku tatu ya kuzibua mishipa ya damu  ambayo imeziba kwa kiwango kikubwa (Chronic Total Occlusion) na hivyo kushindwa kupitisha damu vizuri. …

Soma zaidi »

WAZIRI WA NISHATI AKUTANA NA WAKANDARASI MIRADI YA UMEME VIJIJINI GEITA

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amekutana na wakandarasi wa miradi ya umeme vijijini katika Mkoa wa Geita na kujadiliana kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo kwa ufanisi zaidi. Katika kikao hicho kilichofanyika, Aprili 20, 2019 katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Chato, makubaliano maalum yaliyofikiwa ni kwa wakandarasi husika …

Soma zaidi »