Recent Posts

SERIKALI YA WAKARIBISHA WAWEKEZAJI WA JUMUIYA YA AFASU KUTOKA MISRI

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji imewakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka nchini Misri kupitia Jumuiya ya Muungano Kimataifa chini ya kundi la Afrika na Asia (Afro-Asian Union (AFASU). Ujumbe wa Jumuiya hiyo umefika nchini kwa ajili ya kuangalia fursa za uwekezaji hususani katika sekta ya; Utalii, Kilimo, Afya, …

Soma zaidi »

RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUMSHUSHA MAMA NDOO KICHWANI – MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilwa, kufanya utafiti wa kina wa maeneo ambayo yatawezesha upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yote yenye changamoto ya maji katika wilaya hiyo. Amesema Serikali inayoongozwa na mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuhakikisha huduma ya maji safi …

Soma zaidi »

MHANDISI KUNDO AZINDUA DUKA LA POSTA MTANDAO

Afisa TEHAMA wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Prosper Mallya akimpitisha Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew namna ya kununua gazeti mtandao la kampuni hiyo kabla ya kabla ya uzinduzi rasmi wa Duka Mtandao la Posta ulioambatana na Maadhimisho ya Wiki ya Posta …

Soma zaidi »

WAZIRI MAKAMBA AANZA KUTEKELEZA AGIZO LA MAKAMU WA RAIS MKOANI KIGOMA

Waziri wa Nishati, January Makamba ameanza kutekeleza agizo lililotolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango tarehe 22 Septemba 2021 la kutatua  changamoto ya kukatika umeme mara kwa mara mkoani Kigoma. Katika ziara yake ya kikazi mkoani Kigoma aliyoifanya tarehe 06 Oktoba 2021, Waziri …

Soma zaidi »