Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mussa Sima ameagiza kituo cha kupokea gesi asilia cha Songas eneo la Somanga kuwasilisha mpango kazi wa usimamizi wa mazingira unaoonesha madhara na hatua zinazochukuliwa pindi yanapotokea maafa. Sima alitoa agizo hilo jana wakati wa ziara yake akiwa ameambatana na …
Soma zaidi »TANZANIA NA ANGOLA ZAJADILI USHIRIKIANO KATIKA MAFUTA NA GESI
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amekutana na Balozi wa Angola nchini Tanzania, Sandro De Oliveira na kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano katika utafiti wa Mafuta na Gesi pamoja na ununuzi wa mafuta. Mazungumzo kuhusu ushirikiano huo yalifanyika tarehe 14/11/2019 jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Kaimu Kamishna wa Petroli na Gesi, …
Soma zaidi »GESI TULIYONAYO LAZIMA ITUMIKE KUJENGA UCHUMI WA VIWANDA – DKT KALEMANI
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amesema mpango wa serikali wa miaka 30 wa matumizi sahihi ya rasilimali za gesi na mafuta, pamoja na mambo mengine, umelenga kuhakikisha gesi inatumika kujenga uchumi wa viwanda. Akizungumza katika ufunguzi wa Jukwaa la Tisa la Uziduaji, Novemba 6, mwaka huu jijini Dodoma, Dkt …
Soma zaidi »SERIKALI KUVUNA MABILIONI KUPITIA USAMBAZAJI GESI ASILIA VIWANDANI
Wizara ya Nishati kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), inatarajia kukusanya kati ya shilingi milioni 85 hadi 120 kwa mwezi, sawa na shilingi bilioni 1.02 hadi 1.4 kwa mwaka kutokana na matumizi ya gesi asilia katika kiwanda cha Lodhia kilichopo Mkuranga, ambayo hadi sasa ni futi za ujazo …
Soma zaidi »MRADI WA MATUMIZI YA GESI MAJUMBANI MKOANI MTWARA KUOKOA MAZINGIRA
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema kuwa, mradi wa matumizi ya gesi majumbani ambao utazinduliwa hivi karibuni katika mkoa wa Mtwara utasaidia kuepuka matumizi ya mkaa ambao licha ya kuharibu mazingira, husabisha maradhi mbali mbali. Alisema hayo, Septemba 14, 2019 kwa nyakati tofauti wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani, alipokuwa …
Soma zaidi »MAGARI YANAYOTUMIA GESI YAONGEZEKA NCHINI
Serikali imebainisha kuwa matumizi ya gesi asilia katika magari nchini yamezidi kukua ambapo kwa sasa idadi imefikia 210 kutoka 65 yaliyokuwa yakitumia nishati hiyo, mwaka 2017. Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio, jijini Dodoma, leo Agosti 21, 2019 wakati …
Soma zaidi »TANZANIA NA BRAZIL ZINA MAENEO MENGI YA KUIMARISHA UHUSIANO NA KUENDELEZA MASLAHI YA PAMOJA
Ziara hiyo ya siku kumi imebuniwa na sekta binafsi kwa mashirikiano na ubalozi wa Brazil nchini Tanzania na kuratibiwa kwa pamoja na Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Brasilia, imejumuisha washiriki kumi na mbili ( 12) kutoka wizara …
Soma zaidi »