Maktaba Kiungo: MKOA WA ARUSHA

TANZANIA YAONGEZA HIFADHI SITA KWA KIPINDI CHA MIAKA MITATU

Na Pamela Mollel,Ngorongoro Tanzania imeongeza hifadhi sita (6) kwa kipindi cha miaka mitatu kutoka hifadhi za Taifa 16 hadi 22 hivi sasa. Hayo yalisemwa na Kamishna Mkuu wa shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) Dkt. Allan Kijazi kama moja ya mafanikio kwenye kongamano la watafiti wa masuala ya uhifadhi, kuelekea …

Soma zaidi »

WANACHAMA WA TANZANIA TOUR OPERATORS ASSOCIATION WAKUTANA ARUSHA KUPANGA MIKAKATI YA KUVUTIA WATALII KUTOKA CHINA.

Wanachama wa Tanzania Tour Operators Association (TATO) wakutana Jijini Arusha kupanga mikakati ya kuvutia watalii kutoka China. Mkutano huo umehudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini China  Mbelwa Kairuki na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Nchini(TTB) Jaji Thomas Mihayo na Mkurugenzi wa TTB Bi Devotha Mdachi

Soma zaidi »

WAZIRI UMMY AZINDUA BODI YA TAASISI YA MAENDELEO YA JAMII TENGERU

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameizindua Bodi ya pili ya uendeshaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru na kuitaka kuleta chachu ya mabadiliko katika Sekta ya Maendeleo ya Jamii nchini. Waziri Ummy ameyasema hayo leo Mkoani Arusha wakati akizungumza na wajumbe wa …

Soma zaidi »

WARSHA JUU YA MAJADILIANO YA PAMOJA YA SHERIA MOJA YA UDHIBITI KATIKA UCHIMBAJI WA MADINI YA URANI

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwa kushirikiana na Jumuiya ya Ulaya (EU)  inaendesha warsha ya kuboresha shughuli za kisheria na uhakiki ili kuboresha  uwezo uliopo katika kudhibiti madini ya urani. Warsha hii ya siku tatu ambayo imeanza tarehe 19 hadi  tarehe 21, …

Soma zaidi »

TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA (TAEC) YAIMARISHA UTENDAJI WAKE KWA KUTUMIA TEHAMA

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imetajwa kuongeza tija katika utendaji wake kutokana na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)katika huduma zake kwa wadau. Akizungumza katika kipindi cha “TUNATEKELEZA”   Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Prof. Lazaro Busagali amesema kuwa Tume hiyo imeimarisha utoaji wa huduma zake kwa …

Soma zaidi »

SOKO LA MADINI LAFUNGULIWA RASMI ARUSHA

Waziri wa Madini Dotto Mashaka Biteko amezindua soko la madini mkoani Arusha ambalo litawarahisishia wafanyabiashara na kuruhusu mzunguko wa fedha jambo ambalo serikali imeamua kusimamia rasilimali za nchi Akizungumza katika ufunguzi  wa soko hilo Biteko amesema hakuna serikali inayoweza kujiendesha bila kulipa kodi ambapo maendeleo ya nchi yanaletwa kwa kulipa …

Soma zaidi »

MIRADI 15 YENYE THAMANI YA TSH. BILIONI 22.9 YAZINDULIWA WILAYANI ARUMERU

Mwenge wa Uhuru umemaliza mbio za siku mbili katika halmashauri mbili za wilaya ya Arumeru ambapo jumla ya miradi 15 Kati ya Miradi 16 yenye thamani ya Bilioni 22.9 imezinduliwa, kuwekewa mawe ya msingi, na mingine kukaguliwa na kuangalia uendelevu wake Akihitimisha mbio hizo za mwenge kwa halmashauri ya Meru …

Soma zaidi »

MAWAZIRI WA NISHATI WA AFRIKA MASHARIKI WAAHIRISHA MKUTANO WAO

Mawaziri wenye dhamana na sekta ya nishati kutoka nchi sita zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wameahirisha Mkutano wao uliopangwa kufanyika Arusha, Juni 7 mwaka huu. Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa EAC anayeshughulikia Sekta ya Uzalishaji, Jean Baptiste Havugimana, ilieleza kuwa Mkutano huo utafanyika siku nyingine katika tarehe itakayobainishwa na …

Soma zaidi »

TAASISI ZA FEDHA ZATAKIWA KUCHANGAMKIA VIWANDA VYA USINDIKAJI MAZIWA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo,Profesa Elisante Ole Gabriel amezitaka taasisi za fedha nchini kuchangamkia fursa ya soko la usindikaji wa maziwa ambalo linahitaji uwekezaji wa kimkakati kutokana na sehemu ndogo ya maziwa yanayotoka kwa wafugaji ndiyo yanayosindikwa. Profesa Ole Gabriel ametoa rai hiyo katika kongamano la 10 la Wiki …

Soma zaidi »