Maktaba Kiungo: WIZARA YA AFYA

SERIKALI YAOKOA ZAIDI YA SH. BILION 89 KWA WAGONJWA 5954 WALIOFANYIWA UPASUAJI WA KUFUNGUA NA BILA KUFUNGUA KIFUA KATIKA TAASISI YA MOYO (JKCI)

Kwa kipindi cha miaka minne Serikali imeweza kuokoa zaidi ya shilingi bilioni 89 kwa wagonjwa 5954 wenye matatizo makubwa ya moyo ambao walifanyiwa  upasuaji wa kufungua na bila kufungua kifua katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Kama wagonjwa hawa 5954 waliofanyiwa upasuaji hapa nchini wangetibiwa nje ya nchi Serikali …

Soma zaidi »

JKCI WAFANYA UPASUAJI WA KUTENGANISHA MSHIPA WA DAMU WA KUSAMBAZA DAMU KWENYE MWILI KWA WATOTO

  11/11/2019 Kwa mara ya kwanza madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto  wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wamefanya upasuaji wa kutenganisha mshipa wa damu wa kusambaza damu kwenye mwili na kuweka mshipa bandia wa kusambaza damu kwenye mapafu (Truncus Arteriosus). Upasuaji huo uliochukuwa muda wa masaa …

Soma zaidi »

MAAMBUKIZI YA VVU YAMEPUNGUA KWA WATU WAZIMA KWA ASILIMIA 20.6 NA ASILIMIA 31.3 KWA WATOTO WALIO CHINI YA MIAKA 15 – DKT CHAULA

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula leo amefungua Mkutano wa Makatibu Wakuu wa afya wa  nchin wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo amesema mkutano huo utapitia  ajenda kuu 13 za mkutano zitakazojadiliwa kwenye mkutano wa Mawaziri wa Afya wa nchi za SADC. Akizungumza Dkt …

Soma zaidi »

WANANCHI WENGI WAJITOKEZA KUFANYIWA UCHUNGUZI SARATANI YA MATITI

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania-MEWATA- imefanya zoezi la uchunguzi wa awali wa saratani ya matiti bila malipo kwa lengo la kuongeza uelewa juu ya ugonjwa huo na kuhamasisha jamii umuhimu wa kujichunguza mapema.  Zoezi la uchunguzi limefanyika kwa siku mbili ambapo kina mama …

Soma zaidi »

WATOTO MILIONI 8 KUPATIWA CHANJO YA SURUA-RUBELLA

Inakadiriwa watoto wapatao 8,028,838 wenye umri wa miezi tisa hadi umri wa chini ya miaka mitano (miezi 59) wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya Surua-Rubella kwenye kampeni shirikishi ya chanjo itakayotolewa nchi nzima. Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoro Ummy Mwalimu wakati akizindua kampeni …

Soma zaidi »

SHIRIKISHO LA JAMHURI YA UJERUMANI LIMETOA MSAADA WA EURO MIL 8 KUBORESHA TEKNOLOJIA YA TEHAMA KATIKA MFUKO WA BIMA WA NHIF

Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani limetoa msaada wa Euro milioni 8 ambazo ni sawa na shilingi Bilioni 20 kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwaajili ya kuboresha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika mfuko wa Bima ya Afya nchini NHIF. Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika hafla …

Soma zaidi »

UJERUMANI YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA SH. BIL. 32.7 KUSAIDIA AFYA YA MAMA NA MTOTO

Ujerumani kupitia Benki yake ya Maendeleo (KFW) imeipatia Tanzania msaada wa Euro milioni 13, sawa na sh. bilioni 32.74 kwa ajili ya kuboresha afya ya uzazi na watoto wachanga na pia kukinga maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kupitia mradi ujulikanao kama Tumaini la …

Soma zaidi »

SERIKALI KUSOMESHA MADAKTARI BINGWA 365 KWA AJILI YA KUSAMBAZWA MAENEO YENYE UHABA

  Jumla ya madaktari bingwa 365 wanatarajia kuhitimu mafunzo kuanzia mwaka wa wasomo 2019/2020, 2020/2021 na 2021/2022 ambao watasambazwa kwenye hospitali mbalimbali nchini kulingana na uwiano wa wataalamu waliopo pamoja na kuzingatia maeneo yenye uhaba mkubwa. Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile …

Soma zaidi »