Maktaba Kiungo: WIZARA YA NISHATI

SERIKALI KUPUNGUZA BEI YA KUUNGANISHA UMEME KATIKA MIJI NA MANISPAA

Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu amesema Serikali inaaangalia namna ya kufanya tathmini ya kupunguza bei ya kuunganisha umeme kwa wateja waliopo katika Miji na Manispaa ili huduma hiyo iweze kumfikia kila mmoja na kuondoa malalamiko. Mgalu alisema hayo, Desemba 6,2019, baada ya kubaini  changamoto mbalimbali zilizoibuliwa na wawekezaji na …

Soma zaidi »

UJENZI MRADI WA UMEME RUSUMO WAFIKIA ASILIMIA 59

Mradi wa ujenzi wa kufua umeme wa maji (megawati 80) wa Rusumo, unaotekelezwa kwa ushirikiano wa nchi za Tanzania, Burundi na Rwanda, umefikia asilimia 59 kutoka 32 iliyokuwa imefikiwa Juni mwaka huu. Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti (aliyemaliza muda wake) wa Mawaziri wanaohusika na Mradi huo kutoka nchi husika, ambaye ni …

Soma zaidi »

WAZIRI LUKUVI AWAPA KIBARUA WAKUU WA MIKOA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ametoa wito kwa wakuu wa mikoa kuhakikisha  wanawalinda wamiliki wa ardhi ambao wapo kisheria. Waziri Lukuvi alitoa agizo hilo jana Desemba 05, 2019 wakati wa mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, wafanyabiashara na wawekezaji  uliofanyika mjini Kibaha na  kuongozwa …

Soma zaidi »

AGIZO LA WAZIRI KALEMANI KUPELEKA UMEME KABUKOME LAAMSHA NDEREMO

Wananchi wa kijiji cha Kabukome, Kata ya Nyalubungo, wilayani Biharamulo, Mkoa wa Kagera, wameruka kwa nderemo na vifijo, wakifurahia maagizo aliyoyatoa Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani Desemba 5, 2019, kuwa kijiji hicho kiwe kimewashiwa umeme ifikapo Januari 30 mwakani. Waziri alitoa maagizo hayo mbele ya umati wa wananchi wa …

Soma zaidi »

WAZIRI KALEMANI AKAGUA UJENZI WA KITUO CHA KUPOZA UMEME BULYANHULU NA KUTOA MAELEKEZO

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, Desemba 4, 2019 amekagua maendeleo ya ujenzi unaolenga kupanua kituo cha kupoza umeme Bulyanhulu, wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga na kutoa maelekezo kadhaa kwa uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na mkandarasi husika. Akiwa amefuatana na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha, …

Soma zaidi »

WANANCHI VIJIJINI RUKSA KULIPIA UMEME KWA KUDUNDULIZA

Wananchi wa maeneo ya vijijini ambao hawana uwezo wa kulipia shiingi 27,000 za kuunganishiwa umeme kwa mkupuo, sasa wanaweza kulipia huduma hiyo kwa kudunduliza kidogo kidogo. Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani aliyasema hayo Disemba 3, 2019 kijijini Mnekezi, wilayani Chato, ambapo alikuwa akizungumza na wananchi kabla ya kuwasha rasmi …

Soma zaidi »

TANZANIA NA NAMIBIA WAJADILIANA KUHUSU SACREEE

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na Naibu Waziri wa Nishati wa Namibia, Kornelia Shilunga pamoja na ujumbe wake, wamekutana na kujadili kwa pamoja kuhusu Kituo cha Nishati Jadidifu na matumizi bora ya Nishati cha nchi zilizo Kusini mwa Afrika (SACREEE). Mgalu alikutana na ujumbe huo, Desemba 2, 2019, uliofika …

Soma zaidi »

DKT KALEMANI ATAKA TANESCO IFANYE KAZI KAMA KAMPUNI ZA SIMU

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewaagiza mameneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuwafuata wamiliki wa viwanda, migodi ya madini na hoteli kuwashawishi watumie umeme ili kuzalisha kwa tija hali itakayolipatia shirika hilo mapato zaidi kutokana na malipo ya umeme. Akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ofisini kwa …

Soma zaidi »

BODI YA REA YAMPA SIKU 14 MKANDARASI WA UMEME MKOANI SIMIYU KUJIREKEBISHA

Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imempa siku 14 mkandarasi wa umeme vijijini mkoani Simiyu kuongeza kasi ya usambazaji umeme katika vijiji alivyopangiwa la sivyo Bodi hiyo haitasita kuchukua hatua mbalimbali za kimkataba ikiwemo ya kusitisha mkataba. Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Wakili Julius Kalolo  alisema hayo tarehe 16 …

Soma zaidi »

MKANDARASI WA UMEME WILAYANI CHATO ATEKELEZA MAAGIZO YA BODI YA REA

Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeeleza kuridhishwa kwake na utekelezaji wa maagizo iliyoyatoa kwa Mkandarasi anayefanya kazi ya kusambaza umeme vijijini wilayani Chato kampuni ya Whitecity Guangdong JV ambayo yalilenga kuongeza kasi ya usambazaji umeme vijijini. Hayo yalielezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Wakili Julius Kalolo tarehe …

Soma zaidi »