SPIKA NDUGAI AWAKABIDHI SPIKA WASTAAFU MAJOHO YAO BUNGENI JIJINI DODOMA

3-01
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Bungeni jijini Dodoma, Januari 28, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
7-01
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi kutoka Urambo walioambatana na mbunge wao, Margaret Sitta katika hafla ya kukabidhi majoho kwa Maspika wastaafu iliyofanyika Bugeni jijini Dodoma,Januari 28, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
1-01
Wanakwaya wa Bunge wakiimba Wimbo wa Taifa wakati Spika wa bunge, Job Ndugai alipoafungua Mkutano wa Kumi na Nane wa Bunge jijini Dodoma, Januari 28, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
2-01
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Bungeni jijini Dodoma, Januari 28, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
4-01
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kuteuliwa, Janet Masaburi, Bungeni jijini Dodoma, Januari 28, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
5-01
Spika wa Bunge, Job Ndugai (wa pili kulia) akimvalisha Joho, Spika wa bunge Mstaafu, Pius Msekwa katika hafla ya kukabidhi majoho kwa Maspika Wastaafu iliyofanyika Bungeni jijini Dodoma, Januari 28, 2020. Kulia ni Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
2a-01
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akimkabidhi joho Mhe. Margaret Sitta kwa niaba ya mume wake aliyekuwa Spika wa Bunge la 9 Mhe. Samuel Sitta wakati wa Sherehe fupi za kukabidhiana majoho kwa Maspika wastaafu zilizofanyika  Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai.
2b-01
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akimpa mkono wa pongezi Spika wa Bunge la Kumi Mhe. Anne Makinda baada ya kumkabidhi joho alilokuwa akitumia wakati akiwa Spika wa Bunge la Kumi.PICHA NA BUNGE
2c-01
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) katika picha ya pamoja na Maspika wastaafu ambao ni Mhe. Anne Makinda (wa pili kushoto) na Mhe. Pius Msekwa (wa pili kulia) baada ya Sherehe fupi za kukabidhiana majoho kwa Maspika hao zilizofanyika  Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na Mbunge wa Urambo, Mhe. Margaret Sitta.
7-01
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi kutoka Urambo walioambatana na mbunge wao, Margaret Sitta katika hafla ya kukabidhi majoho kwa Maspika wastaafu iliyofanyika Bugeni jijini Dodoma, Januari 28, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI MKUU AMPONGEZA BONDIA SALIM MTANGO ALIYESHINDA MKANDA WA DUNIA WA UBO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *