UJENZI WA VIVUKO BUGOROLA UKARA, CHATO NKOME KUKAMILIKA AGOSTI

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle wa pili kushoto akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala huo Prof. Idrissa Mshoro wa pili kulia wakati wakikagua maendeleo ya ujenzi wa vivuko vya Bugorola Ukara na Chato Nkome katika tukio lilofanyika katika yadi ya Songoro. Ujenzi wa vivuko hivyo unategemewa kukamilika ifikapo mwezi Agosti mwaka huu, ujenzi huo umechelewa kukamilika kama ilivopangwa kutokana na kutokea kwa ugonjwa wa mafua makali maarufu Covid 19. Kulia ni meneja wa TEMESA Mwanza Mhandisi Hassan Karonda na kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni ya Songoro inayojenga vivuko hivyo Major Songoro.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle kushoto, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala huo Prof. Idrissa Mshoro katikati na Mkurugenzi wa kampuni ya Songoro Major Songoro wakipita pembeni ya kivuko kinachotarajiwa kutoa huduma kati ya Bugorola na Ukara wakati walipokua wakikagua maendeleo ya ujenzi wa vivuko ambavyo vinatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Agosti mwaka huu. Tukio hilo lilifanyika katikayadi ya Songoro iliyopo Ilemela.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle kulia akimueleza jambo Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala huo Prof. Idrissa Mshoro wa pili kulia wakati alipotembelea karakana hiyo kujionea maendeleo ya ujenzi na ukarabati wa karakana hiyo unavyoendelea. Wa tatu kulia ni meneja wa TEMESA Mwanza Mhandisi Hassan Karonda.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle aliyenyoosha mkono akimuonyesha maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa majengo mapya ya karakana ya mkoa wa Mwanza Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala huo Prof. Idrissa Mshoro wa pili kulia wakati alipotembelea karakana hiyo kujionea ujenzi unavyoendelea. Kulia ni meneja wa TEMESA Mwanza Mhandisi Hassan Karonda.

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUMSHUSHA MAMA NDOO KICHWANI – MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilwa, kufanya utafiti wa kina …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.