Documentary – SAFARI YA MAISHA BORA

Ni Safari ya Kutembelea Maeneo ya Mradi ya Kitwai, Saunyi na Msomera.

Serikali imeendelea kutoa elimu na kuwashawishi wananchi kuhama kwa hiari ndani ya eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, ambapo Tarehe 14, Septemba 2024 Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro iliandaa safari ya wawakilishi wa wananchi wakiwemo viongozi, malaigwanani na wakaazi wa Ngorongoro kwenda kutembelea na kujionea maeneo yaliyotengwa na Serikali ili kufanya uamuzi sahihi.

Ad

Safari hii ilianza mapema asubuhi kutoka Wilaya ya Karatu (Mkoa wa Arusha), kupitia Wilaya za Simajiro (Mkoani Manyara), Kilindi na kuhitimishwa eneo la Msomera lililopo Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mama Mzazi wa Mama Janeth Magufuli (Juliana Stephano Kidaso) katika eneo la Kigongo Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *