WIZARA YA AFYA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Waziri wa Afya Jenista Mhagama mara baada ya kushiriki Adhimisho la Misa Takatifu ya Sherehe ya Bikira Maria Mama wa Mungu na Mwaka Mpya 2025 iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege Dodoma tarehe 01 Januari 2025

Soma zaidi »

Tunawatakia Watanzania Wote Heri ya Mwaka Mpya 2025 Salamu za heri na mafanikio kwa Watanzania wote. Katika mwaka huu mpya, tunataka kila Mtanzania aendelee kufurahia maendeleo, amani, na mshikamano. Tukiwa na umoja, nguvu na nia ya kujenga taifa letu, tunaamini tutapata mafanikio makubwa zaidi katika sekta zote, ikiwa ni pamoja na elimu, afya, uchumi, na miundombinu

Mwaka 2025 ni fursa nyingine ya kuendelea kujenga taifa lenye neema, lenye kujivunia na lililo na ustawi kwa kila mmoja wetu. Heri ya mwaka mpya kwa Watanzania wote, kwa familia zenu na kwa jamii nzima ya Tanzania. #HeriYaMwakaMpya #MatokeoChanya+ #TanzaniaKwanza

Soma zaidi »

Ushirikiano wa Wananchi na Serikali katika Kuboresha Huduma za Afya

Kituo cha Afya Kafita, kilichopo katika Wilaya ya Nyang’hwale, Kata ya Kafita, kijiji cha Kafita, ni mfano wa mafanikio ya ushirikiano kati ya wananchi, Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), na serikali kuu. Ujenzi wa kituo hiki umegharimu jumla ya shilingi milioni 200, fedha ambazo zilitokana na juhudi za wananchi, …

Soma zaidi »

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameviagiza vyombo vyote vya usalama vihakikishe watu wote waliokwama ndani ya jengo lililoporomoka katika kata ya Kariakoo jijini Dar es Salaam wanaokolewa huku mali zao zikilindwa.

Ametoa agizo hilo (Jumamosi, Novemba 16, 2024) baada ya kushuhudia juhudi za uokoaji zinavyoendelea baada ya jengo ghorofa nne kuporomoka katika eneo la Karikoo. Akizungumza baada ya kukagua juhudi za uokoaji katika eneo hilo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Majaliwa amesema hadi sasa watu 40 mejeruhiwa ambapo …

Soma zaidi »

“Mhe Rais nikupe habari njema…..”

“Mhe Rais nikupe habari njema; picha yako hiyo.. (picha ya Rais Dkt. Samia akiwa katika chumba Maalum cha kuokolea maisha watoto wachanga wanaozaliwa na changamoto za kiafya, alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi 14/07/2024), Mhe Rais picha yako hiyo imenipa (Wizara ya Afya) ahadi ya kupata Dola za …

Soma zaidi »

WAZIRI MKUU: SERIKALI IMEIMARISHA NGUVUKAZI SEKTA YA AFYA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeimarisha nguvukazi kwenye sekta ya afya kwa kuongeza taasisi zinazotoa mafunzo ya afya na upatikanaji wa fursa za elimu ya juu kwa kada hiyo. “Serikali imefanya upanuzi wa taasisi za mafunzo ya afya ili kuongeza idadi ya wahitimu. Taasisi hizo ni pamoja na vyuo …

Soma zaidi »

RAIS SAMIA ATEMBELEA RUKWA.. AANGAZIA AFYA, ELIMU, KILIMO NA MIUNDOMBINU KWA MIRADI YA MAENDELEO.

Katika ziara ya Rais Samia siku ya leo iliangazia kwenye sekta ya Afya, Elimu, Kilimo na Miundombinu kwa kufanya upanuzi wa Hospital za wilaya za Sumbawanga Bilioni 13.7, Ujenzi wa vituo vya Afya 21 na zahanati 30 kwa gharama ya bilioni 9.4, Elimu ya ngazi chini shule mpya za msingi …

Soma zaidi »

Maendeleo Ya Huduma Za Kijamii Zafufua Tumaini Jipya Mkoani Katavi..

Maendeleo ya huduma za kijamii yameleta matumaini mapya kwa wakazi wa mkoa wa Katavi. Huduma hizi zimeboreshwa kwa kiwango kikubwa, na kufanikisha uimarishaji wa miundombinu ya afya, elimu, na maji safi, ambayo imekuwa ni changamoto kwa muda mrefu katika mkoa huu. 1.Sekta ya Afya Hospitali ya mkoa wa Katavi imeboreshwa …

Soma zaidi »

MAENDELEO MAKUBWA, HOSPITALI YA MKOA WA KATAVI YAZIDI KUNG’ARA KATIKA SEKTA YA AFYA

Mkoa wa Katavi umeandika historia mpya katika sekta ya afya kupitia maendeleo makubwa yanayoshuhudiwa katika Hospitali ya Mkoa. Hospitali ya Mkoa ya Katavi imekuwa kielelezo cha mafanikio na maendeleo katika utoaji wa huduma bora za afya kwa wakazi wa mkoa huo. Hii ni hatua muhimu inayolenga kuboresha afya na ustawi …

Soma zaidi »