Waziri Mkuu

Mhe Kassim Majaliwa Akiweka Jiwe La Msingi La Hospitali Kaskazini Unguja

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Januari 11, 2024 ameweka jiwe la msingi la Hospitali ya Wilaya ya Kaskazini “B”- Pangatupu, Mkoa wa Kaskazini Unguja, ujenzi wake umegharimu Tsh Bil. 6.7. Hii ni sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Soma zaidi »

PIKIPIKI ZILIZOTELEKEZWA KWA MIAKA MITATU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua pikipiki zilizotelekezwa kwenye stoo ya Wakala wa Maji na usafi na Mazingira Vijijini, Mkoa wa Lindi, alipofanya ziara katika ofisi zao. Pikipiki hizo zilinunuliwa mwaka 2021 kwa ajili ya kuzigawa kwa Jumuiya za Watumiaji maji Mkoa wa Lindi.

Soma zaidi »

TANZANIA KUISAIDIA MSUMBIJI KUKOMESHA VITENDO VYA KIGAIDI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Tanzania itandelea kuwa mstari wa mbele kuisaidia nchi ya Msumbiji katika kukabiliana na vitendo ya kigaidi katika nchi hiyo. Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Machi 24, 2022) alipomuwakilisha Rais  Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa kujadili usalama katika eneo la Kusini Mashariki mwa Afrika hususan nchini …

Soma zaidi »

RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUMSHUSHA MAMA NDOO KICHWANI – MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilwa, kufanya utafiti wa kina wa maeneo ambayo yatawezesha upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yote yenye changamoto ya maji katika wilaya hiyo. Amesema Serikali inayoongozwa na mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuhakikisha huduma ya maji safi …

Soma zaidi »

RAIS SAMIA AMEDHAMIRIA KUTEKELEZA MRADI WA LNG – MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kwa dhati kuhakikisha kuwa mradi wa kusindika gesi asilia kuwa kimiminika (LNG) utakaogharimu Dola za Kimarekani bilioni 30 sawa na takriban shilingi trilioni 70, unaanza kazi ili kuleta manufaa kwa wananchi. Majaliwa ameyasema hayo (Jumanne, Oktoba 5, 2021) wakati akizungumza na wananchi katika …

Soma zaidi »

SERIKALI YAZIAGIZA TAASISI ZA FEDHA KUWAWEZESHA WAFANYABIASHARA VIJIJINI

Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imezungumza na taasisi za fedha na zile zinazosaidia kuwezesha wananchi kiuchumi ili kuwawezesha wafanyabiashara wa vijijini. Hatua hiyo itatatua changamoto ya upatikanaji wa kiwango kidogo cha fedha katika maeneo hayo hivyo kuwawezesha wafanyabishara wanaowekeza vijijini kuendelea. Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Waziri Mkuu, …

Soma zaidi »

TANGULIZENI MASLAHI YA TAIFA – WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mabalozi wanaoteuliwa kuiwakilisha Tanzania nje ya nchi wanapaswa kutanguliza maslahi ya Taifa katika utekelezaji wa majukumu yao. Amesema kuwa mabalozi hao wanapaswa kutekeleza falsafa ya Mheshimiwa Rais Samia ya kuona kazi zilizoratibiwa zinaendelea kutekelezwa kwa uadilifu mkubwa na uaminifu ili ziweze kutoa matokeo chanya katika …

Soma zaidi »