ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar wakati akitokea Harare nchini Zimbabwe

Mhe. Rais Dkt. Samia alishiriki Mkutano wa 44 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya hiyo (SADC-Organ Troika)

Soma zaidi »

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameondoka Zanzibar na kuelekea Dodoma leo

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Makamu wa Pili wa Rais, Mhe. Hemed Suleiman Abdallah, ameongoza Watendaji Wakuu wa Serikali kumuaga Rais Dk. Mwinyi. Akiwa Mjini Dodoma, Rais Mwinyi anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano wa Baraza Kuu la Kanisa la Tanzania Assemblies of God, Chuo …

Soma zaidi »

RAIS DK. MWINYI; ZANZIBAR KUPUNGUZIWA GHARAMA ZA UENDESHAJI WA MIRADI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameonesha utayari wa Serikali ya Zanzibar kushirikiana na Taasisi ya Mabenki Yasiyo na Mipaka (Bankers without Boundaries) katika kuwekeza kwenye miradi ya kipaumbele ambayo italeta tija kwa nchi. Dk. Mwinyi alitoa kauli hiyo leo, tarehe 14 …

Soma zaidi »

Mafanikio Na Umuhimu Wa Muungano Wa Tanzania: Sababu Za Kuunganisha Tanganyika Na Zanzibar

Kuunganisha Tanganyika na Zanzibar kulilenga kujenga umoja wa kitaifa na kuvunja mipaka ya kikanda na kikabila. Hii ilikuwa hatua muhimu katika kujenga utambulisho mpya wa kitaifa ambao ungeweza kuunganisha wananchi wa Tanzania kama taifa moja lenye lengo la pamoja. Kuleta Utulivu na Amani: Muungano ulikuwa ni jitihada za kuzuia migogoro …

Soma zaidi »

Historia ya Umoja: Kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya Tanganyika na Zanzibar

Historia ya Muungano wa Tanzania ni hadithi ya ujumuishaji wa mataifa mawili ya Tanganyika na Zanzibar kuwa taifa moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Muungano huu ulianzishwa rasmi tarehe 26 Aprili 1964 na kufuatia Mkataba wa Muungano uliosainiwa baina ya Serikali ya Tanganyika chini ya Mwalimu Julius Nyerere na …

Soma zaidi »

 Je, Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi wa Zanzibar anawezaje kuunganisha maadili, uwajibikaji, na maendeleo kwa ustawi wa Zanzibar?

Falsafa za uongozi wa Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi wa Zanzibar zinajikita katika maadili, uwajibikaji, na maendeleo endelevu Uwajibikaji na Uadilifu Rais Mwinyi anasisitiza uwajibikaji na uadilifu katika uongozi wake. Anaamini kwamba viongozi wanapaswa kuwa mfano bora wa kuigwa kwa wananchi na kutekeleza majukumu yao kwa uwazi na haki. Ushirikiano …

Soma zaidi »

USHAWISHI WA TANZANIA DUNIANI UTATEGEMEA NA UBORA WA SERA YA MAMBO YA NJE INAYOREKEBISHWA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu-Zanzibar, Mhe.  Ali Suleiman Ameir akitoa hotuba ya ufunguzi ya Kongamano la Wadau kuhusu kukusanya maoni ya marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 lililofanyika Hoteli ya Golden Tulip mjini Zanzibar tarehe 05 Februari 2024. Waziri wa Mambo ya Nje na …

Soma zaidi »