Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa Baraza la Mawaziri utasaidia kuboresha utendaji kazi na kuleta ufanisi zaidi katika kuwahudumia wananchi

Amesema kuwa maboresho hayo ya matumizi ya mfumo wa kielektroniki yatasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matumizi ya karatasi katika vikao vya Serikali, hususan Baraza la Mawaziri, hivyo kupunguza changamoto ikiwemo kuchelewa kwa taarifa, gharama kubwa za uchapaji na hatari ya upotevu wa taarifa muhimu.

Amesema hayo leo (Jumatatu, Novemba 11, 2024) wakati akifunga Mkutano wa Kazi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri kuhusu matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa Baraza La Mawaziri (e-CABINET), kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

Ad

Ameongeza kuwa hatua hiyo inatokana na jitihada na malengo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kusisitiza umuhimu wa Mawaziri na watumishi wa umma kuzingatia mabadiliko ya kiteknolojia katika utendaji kazi,

“Matokeo ya mwaka 2023 ya ulinganifu baina ya nchi katika muktadha wa Ukomavu wa Matumizi ya Teknolojia Serikalini (Government Technical Maturity Index), nchi yetu ilishika nafasi ya tatu (3) ikilinganishwa na nchi nyingine Barani Afrika. “Tunampongeza na kumtakia kila la kheri Rais Dkt. Samia aendelee kubuni zaidi kwa manufaa ya Taifa letu .

” Kadhalika, Waziri Mkuu amesema kuwa mkutano huo kuhusu matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa Baraza la Mawaziri ni sehemu ya juhudi za serikali katika kuhakikisha kwamba Mawaziri na watumishi wa umma wanakuwa na ujuzi wa kisasa wa uendeshaji wa shughuli za Serikali na utumishi kwa ujumla.

Kwa Upande wake, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amewapongeza wataalam kutoka Wakala wa Serikali Mtandao kwa kufanikisha mafunzo hayo. “Tunaamini tumeelewa kwa kiwango kikubwa sana. ”

Ad

Unaweza kuangalia pia

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdory Mpango, tarehe 01 Novemba 2024 ameungana na kuongoza Waombolezaji Katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo,jijini Dar-es-Salaam, kuaga mwili wa marehemu Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali David Bugozi Musuguri

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *