Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi ametembelea kaburi la aliyekuwa Rais wa Awamu ya 3, hayati Benjamin William Mkapa katika Kijiji cha Lupaso mkoani Mtwara, Julai 28, 2024, kuhani familia na kuzungumza na wananchi wa Lupaso.

Balozi Nchimbi amesema “naomba nikiri kuwa mimi ni mwanafunzi wa hayati na nimekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa (UVCCM), katika kipindi chake. Ndiye alinilipia ada ya kusoma chuo kikuu na alikuwa mfuatiliaji sana na alitulea vizuri. Sio sisi tu, bali Watanzania wote aliwalea pia. Alikuwa mzalendo kwa nchi, alifanya mabadiliko makubwa kwa nchi yake na kwa Chama chake, lakini yote CCM chini ya Dkt Samia tutaendelea kuyaenzi yale yote aliyoyoacha hayati Benjamin Mkapa. Pamoja hayo nimeambiwa kero za hapa na tumezichukua. CCM inatoa shilingi milioni 10 kuanza kukarabati shule ya hapa Lupaso.

” Katika ziara hii Dk Nchimbi ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amosi Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni Ndg. Issa Ussi Haji (Gavu) pamoja na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Rabia Abdallah Hamid.

Ad
Ad

Unaweza kuangalia pia

TRENI YA MCHONGOKO YAANZA SAFARI KWA KISHINDO DAR – DOM

Treni ya Umeme ya Kisasa (EMU) ya Reli ya Kisasa (SGR) nchini Tanzania ni sehemu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *