MatokeoChanya

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AONGOZA KIKAO CHA MASHAURIANO CHA VYAMA VYA SIASA WANACHAMA WA TCD.

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, akiongoza Kikao cha Mashauriano cha Vyama vya Siasa Wanachama wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), ambacho, mbali ya viongozi wa vyama hivyo, pia kilihudhuriwa na mawaziri na manaibu waziri wakiwakilisha upande wa Serikali. Baadhi ya viongozi wakuu wa vyama hivyo walioshiriki …

Soma zaidi »

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar wakati akitokea Harare nchini Zimbabwe

Mhe. Rais Dkt. Samia alishiriki Mkutano wa 44 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya hiyo (SADC-Organ Troika)

Soma zaidi »

Rais Samia, Rais aliyeleta mageuzi

Mageuzi yana nafasi muhimu katika kuboresha mifumo ya kiutawala, kiuchumi, na kijamii, kama inavyotamkwa katika Katiba ya Tanzania. Katiba inaelekeza kwamba serikali ina wajibu wa kuhakikisha kuwa rasilimali za taifa zinatumiwa kwa manufaa ya Watanzania wote na kwamba kuna uwazi na uwajibikaji katika utendaji wa shughuli za serikali. Rais Samia …

Soma zaidi »

Rais Samia, Rais Wa Maridhiano

Maridhiano ni mojawapo ya nguzo kuu za demokrasia ambayo imeainishwa katika Katiba ya Tanzania, hususan kwa kuhakikisha kuwa haki na uhuru wa kila raia vinaheshimiwa (Sehemu ya Tatu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977). Rais Samia, kupitia sera ya maridhiano, anajenga msingi wa umoja wa kitaifa kwa …

Soma zaidi »

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania katika ziara maalumu ya kuboresha mahusiano nchini Cuba

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania iko tayari kushirikiana na Serikali ya Cuba kujenga kiwanda kikubwa cha kuzalisha chanjo mbalimbali ikiwemo chanjo ya homa ya ini. Amesema viwanda vya dawa nchini Cuba vikiwemo vinavyotengeneza dawa zinazotokana na mimea tiba vimeiwezesha nchi hiyo kupunguza utegemezi wa kuagiza dawa kutoka …

Soma zaidi »

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Gabriel Mugabe kwa ajilli ya kushiriki Mkutano wa 44 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Harare nchini Zimbabwe

#MSLAC #SisiNdioWajenziWaTanzaniaYetu #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya #MSLAC #SamiaSuluhuHassan #ChamaChaMapinduzi #PhilipMpango #wizarayaafya #wizarayaujenzi

Soma zaidi »

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Mawaziri kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam

Mawaziri hao walioapa ni: Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Mb.) kuwa Waziri wa Katiba na Sheria; Mhe. William Vangimembe Lukuvi (Mb.) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu); Mhe. Jenista Joackim Mhagama (Mb.) kuwa Waziri wa Afya; na Mhe. Balozi Dkt. Pindi Hazara …

Soma zaidi »

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameondoka Zanzibar na kuelekea Dodoma leo

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Makamu wa Pili wa Rais, Mhe. Hemed Suleiman Abdallah, ameongoza Watendaji Wakuu wa Serikali kumuaga Rais Dk. Mwinyi. Akiwa Mjini Dodoma, Rais Mwinyi anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano wa Baraza Kuu la Kanisa la Tanzania Assemblies of God, Chuo …

Soma zaidi »