MatokeoChanya

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Sekretariet ya Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) wakiongozwa na Mkurugenzi wa Masuala ya Ushirikiano katika Usimamizi na Menejimenti ya Taka za Plastiki Bi. Clemence Schmid, Chamwino Dodoma

Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais amesema serikali imedhamiria kushirikiana na wadau, sekta binafsi pamoja na jumuiya ya kimataifa katika kupambana na tatizo la taka za plastiki nchini. Amesema uzoefu unaonesha kwamba ushirikiano ni njia bora zaidi itakayowezesha kukabiliana na tatizo hilo kwani yapo maeneo ambayo taka za plastiki hutupwa …

Soma zaidi »

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Mhe. Ronald Lamola na Waziri wa Mambo ya Nje wa Madagascar, Mhe. Dkt. Rasata Rafaravavitafika pembezoni mwa Mkutano wa Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Harare, Zimbabwe.

Akizungumza na Mhe. Lamola, Waziri Kombo ameeleza kuwa Tanzania itaendelea kudumisha ushirikiano wa kihistoria na kindugu uliopo baina ya Tanzania na Afrika kusini ili kukuza sekta za kiuchumi ikiwemo biashara, utalii, uwekezaji, elimu, afya na maeneo mengine ya kimkakati kwa maslahi ya pande zote mbili.   Naye Mhe. Lamola ameeleza …

Soma zaidi »

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amepokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Jamhuri ya Mali, Mheshimiwa Madou Diallo.

Balozi Diallo amemshukuru Rais Samia kwa mapokezi mazuri na kueleza dhamira yake ya kuendeleza na kukuza mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Mali. Amesisitiza kwamba atafanya kazi kwa bidii kuhakikisha kuwa nchi hizi mbili zinanufaika na ushirikiano wao katika nyanja mbalimbali. Mheshimiwa Diallo, ambaye atakuwa na makazi yake jijini Addis …

Soma zaidi »

RAIS DK. MWINYI; ZANZIBAR KUPUNGUZIWA GHARAMA ZA UENDESHAJI WA MIRADI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameonesha utayari wa Serikali ya Zanzibar kushirikiana na Taasisi ya Mabenki Yasiyo na Mipaka (Bankers without Boundaries) katika kuwekeza kwenye miradi ya kipaumbele ambayo italeta tija kwa nchi. Dk. Mwinyi alitoa kauli hiyo leo, tarehe 14 …

Soma zaidi »

CP DKT. KYOGO: POLISI WAPO KWA AJILI YA KULINDA USALAMA WENU, USHIRIKIANO MUHIMU KUELEKEA UCHAGUZI

“Polisi wako hapa kwa ajili yenu, siyo kuwafanyia vitisho bali kuhakikisha usalama wenu unadumishwa. Tunahitaji ushirikiano wenu ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na uadilifu,” CP Dkt . Ezekieli Kyogo Aliongeza kuwa, ni muhimu kwa wananchi wote kushirikiana na polisi katika kupambana na uhalifu, hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi …

Soma zaidi »

WATANZANIA WAPONGEZA UBORA WA TRENI YA SGR, MRADI ULIOLETA AJIRA NA KUBORESHWA KWA USAFIRI NCHINI

Wananchi wa Tanzania wameonyesha furaha na shukrani kwa serikali kutokana na ujenzi wa treni ya SGR, mradi ambao umeleta mabadiliko makubwa katika sekta ya usafiri nchini. Treni ya SGR inasifika kwa ubora wake, ikiwa na miundombinu ya kisasa inayorahisisha safari kwa muda mfupi na kwa usalama wa hali ya juu. …

Soma zaidi »