RAIS SAMIA AKIPOKEA RIPOTI YA (CAG) NA TAARIFA YA UTENDAJI KAZI WA (TAKUKURU) KWA MWAKA 2022/2023

“Ripoti hizi zilizotolewa hapa zinasaidia katika maboresho ya serikali kwa watumishi wa umma kwasababu ripoti zilizotolewa hapa tutakwenda kuangalia kwenye dosari na kufanya marekebisho na mwakani pengine hizi hazitajirudia na tutakuwa tumesogea.

Tunawashukuru sana CAG na TAKUKURU kwakuwa kazi hii inaimarisha utendaji ndani ya mashirika ya umma na kupunguza hasara…itafika pahali mashirika yetu hayatakuwa kwenye hasara na badala yale yataleta faida.

Ad

Tumesikia ongezeko la hati safi na hii ni kwasababu CAG anatoa hati hapa na watu wakipata wanakwenda kurekebisha na matokeo yake tuna 99% ya hati safi na 1% ndio hati chafu kwahiyo tunasinga mbele ripoti hizi zinatusaidia sana.

Ripoti hizi zinatusaidia kwenye kungeza ukusanyaji wa mapato na tumeona vipengele mbalimbali vya CAG na TAKUKURU kwamba wanasaidia kuziba ile mianya ya kupotea kwa fedha na rushwa na mapato kurudi serikali na hii inasiaida kuimarisha nidhamu katika matumizi ya serikali na utendaji kazi wetu.

Naipongeza TAKUKURU kwa ubunifu mpya wa uibuaji wa kero kwa kushirikiana na wananchi kwamba wanakwenda kule chini wanakaa na wananchi na wananchi wanasema na wao wanazichukua kero wnazipeleka taasisi husika zinafanyiwa kazi na hii inatusaidia kupunguza kero kwa wananchi na kutufanya serikali iwajibike ipasvyo.

Nimpongeze CAG kwa uibuaji wa mambo kadhaa na kupendekeza hatua za kuchukiliwa ingawa ametuhimiza kwamba utekelezaji uende kwa haraka na kwa kiwango kikubwa lakini yote hayo yanatusaidia kwenda kutekeleza yale maelekezo ambayo CAG na TAKUKURU wanayaibua huko wanapofanya kazi kuyaleta Serikalini.

Kwa ujumla nishukuru kazi kubwa sana inayofanywa na Taasisi hizi mbili na kwa mujibu wa katiba kazi yangu leo hapa ni kupokea ripoti ya CAG lakini safari haijaisha, katiba inanitaka ninapozipokea ndani ya muda fulani niwe nimezikabidhisha Bungeni nami nakuahidi nitafanya hivyo CAG.

Kwa upande wa taarifa za TAKUKURU tutazifanyia kazi ndani ya Serikali na maeneo yote yaliyoibuliwa tutayafanyia kazi ipasavyo.

Wakati taarifa zinawasilisha nilikuwa natizama sura za watu tumechoka kwelikweli nadhani kwasababu Alhmis lakini pia yaliyokuwa yakisemwa ni makubwa pia, lakini kuna swahum na kwaresma, sasa wale wa kwaresma karibu mnafunguka mnamaliza niwatakie Pasaka njema, twendeni tusherehekee Pasaka kwa usalama…wale wa swahum tuendelee hatupo mbali inatelemka kwa kasi…tunakwenda vizuri.”

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

#Na Haya Ndiyo Matokeo Chanya+

Ad

Unaweza kuangalia pia

Serikali ya Tanzania na Czech Zakubaliana Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili

Serikali za Tanzania na Czech kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kuvutia uwekezaji kati yao. Kuondoa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *