Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Mhe. Ronald Lamola na Waziri wa Mambo ya Nje wa Madagascar, Mhe. Dkt. Rasata Rafaravavitafika pembezoni mwa Mkutano wa Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Harare, Zimbabwe.

Akizungumza na Mhe. Lamola, Waziri Kombo ameeleza kuwa Tanzania itaendelea kudumisha ushirikiano wa kihistoria na kindugu uliopo baina ya Tanzania na Afrika kusini ili kukuza sekta za kiuchumi ikiwemo biashara, utalii, uwekezaji, elimu, afya na maeneo mengine ya kimkakati kwa maslahi ya pande zote mbili.  

Naye Mhe. Lamola ameeleza kuwa Afrika Kusini inaendelea kuthamini mchango wa Tanzania katika harakati za ukombozi wa Taifa hilo hivyo, ina nia ya dhati ya kuuenzi mchango huo kwa kukuza ushirikiano katika shughuli za kiuchumi, kijamii na kisiasa kwa ustawi wa wananchi wa mataifa hayo mawili.

Ad

Aidha, katika mazungumzo ya Mhe. Kombo na Mhe. Dkt. Rafaravavitafika wamejadili juu ya kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kiuchumi na taifa hilo hususan katika sekta ya uchumi wa blue ambao Tanzania imeuwekea mkazo ili kukuza uchumi kupitia rasilimali za bahari zinazopatikana na kukuza biashara yake kimataifa.

Image

Ad

Unaweza kuangalia pia

Tanzania Yapiga Hatua Kubwa katika Miradi ya Maji, Zaidi ya Miradi 1,500 Yakamilika Vijijini na Mijini.

Tanzania imefanya maendeleo makubwa katika miradi ya maji, na hadi sasa, miradi mingi imekamilika ili …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *