Maktaba Kiungo: UTALII TANZANIA

WAMILIKI WA VIWANDA VYA MISITU WAHAKIKISHIWA KUONGEZEWA MIKATABA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii. Mhe. Constantine Kanyasu amewahakikishia wamiliki wa viwanda vya misitu Tanzania kuwa atashughulikia ombi lao la kutaka kuongezewa muda wa mikataba yao kutoka  miaka miwili hadi  mitano ya kupewa mgao wa vitalu vya miti Pia ameahidi kuyafanyia kazi malalamiko mbalimbali yaliyowasilishwa ofisini kwake na wamiliki …

Soma zaidi »

WAZIRI MKUU KUWAPOKEA WATALII 300 KUTOKA CHINA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameahidi kupokea kundi la watalii wasiopungua 300 ambao wanatarajiwa kuwasili nchini Machi, mwaka huu. Watalii hao ni kundi la kwanza miongoni mwa watalii 10,000 wanaotarajiwa kuwasili nchini katika mwaka 2019 chini ya mpango unaosimamiwa baina ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Bodi ya Utalii Tanzania na …

Soma zaidi »

WAZIRI MKUU APOKEA LESENI YA USAJILI WA TANZANIA SAFARI CHANNEL

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea leseni ya usajili wa chaneli ya utalii ya Tanzania Safari ambayo itaiwezesha kuoneshwa kwa umma bila ya malipo yoyote (a must-carry channel) na wamiliki wa visimbusi. Waziri Mkuu amekabidhiwa leseni hiyo leo mchana (Jumatano, 16 Januari, 2019) kwenye kikao alichokiitisha ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma …

Soma zaidi »

NAIBU WAZIRI, KANYASU ATEMBELEA IHUMWA MJI WA SERIKALI KUKAGUA UJENZI JENGO LA MALIASILI NA UTALII

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu amesema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii linalojengwa ndani ya mji wa Serikali katika eneo la Ihumwa Jijini Dodoma. Ameyabainisha hayo wakati alipotembelea eneo hilo kwa ajili ya kukagua maendeleo yaliyofikiwa katika ujenzi …

Soma zaidi »

NAIBU WAZIRI KANYASU AWATAKA WANANCHI WANAOISHI NDANI YA HIFADHI YA MISITU KULIPA TOZO BILA SHURUTI

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu amewataka wananchi wanaoishi na kufanya shughuli za uzalishaji mali ndani  ya Hifadhi ya misitu ya Visiwa vya  Kome  na Maisome vilivyoko wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza kulipa tozo za serikali bila kulazimishwa. Kauli hiyo ameitoa  wakati alipokuwa akizungumza na wakazi wanaoishi …

Soma zaidi »

“SERIKALI YETU INATUJALI NA KUTUPENDA SANA” – DIAMOND PLATNUMZ

  Afanya mahojiano na waandishi wa habari jijini Nairobi. Azungumzia tatizo lililotokea katika onesho la Mwanza na kukiri kuwa yeye na wasanii wenzake walikosea na serikali imewasikiliza na kuwasamehe. Aeleza taratibu walizoelekezwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kumaliza kosa walilofanya na namna wanavyolitekeleza. Sasa Wasafi Festival 2018 kuendelea …

Soma zaidi »