Kamati ya Pili ya Mchanga wa Madini kuwasilisha ripoti yake kwa Rais Magufuli Jumatatu 12 Juni, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli atapokea taarifa ya kamati ya pili ya wachumi na wanasheria iliyofanya uchunguzi madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga wa madini yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini Jumatatu tarehe 12 Juni, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Tukio hili litarushwa hewani moja kwa moja (Mubashara) kupitia vyombo mbalimbali vya habari vya redio, televisheni, mitandao ya kijamii na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz kuanzia saa 3:30 Asubuhi.

Ad

Wananchi wote mnakaribishwa kufuatilia matangazo hayo kupitia vyombo vya mbalimbali vya habari ama simu zenu za mikononi kwa kutembelea tovuti rasmi ya Ikulu iliyotajwa hapo juu.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
10 Juni, 2017

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *