Jengo lililofungwa rada mpya kwa ajili ya kuongozea ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

TCAA KUFANYA MAJARIBIO YA KWANZA YA MFUMO WA RADA

Msimamizi wa Ujenzi wa jengo
Msimamizi wa Ujenzi wa jengo lililokuwa ikifungwa rada hiyo jijini Dar es Salaam, Steven Mwakisasa akitoa ufafanuzi juu ya masuala yanayohusu ujenzi huo.
  • Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), inatarajia kufanya majaribio ya kwanza ya mfumo wa rada ya kuongozea ndege nchini unaojengwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
 Mmoja ya wanamama muongoza Ndege Bi. Mossy Kitang'ita akiwajibika.
Mmoja ya wanamama muongoza Ndege Bi. Mossy Kitang’ita akiwajibika.
  • Akizungumza na wanahabari waliofanya ziara ya kutembelea ujenzi huo, Msimamizi wa Ujenzi wa jengo lililokuwa ikifungwa rada hiyo jijini Dar es Salaam, Steven Mwakisasa amesema ujenzi wa jengo hilo umekamilika na ufungaji wa vifaa unaendelea hivyo ifikapo Desema 21 wataweza kufanya majaribio.
  • “Kama mnavyoona wanahabari kila kitu kimeshafanyika tunachomalizia ni mitambo midogo midogo inayotarajia kukamilika ifikapo wiki ijayo na tufanye majaribio ili kuona ni wapi pa kurekebisha au tuongeze kitu gani?,” amesema Mwakisasa.
RADA
Wanahabari waliofanya ziara katika mnara wa kuongozea ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.
  • Nae mwongoza Ndege Mkuu wa TCAA, Justine Ncheye amesema mara baada ya kukamilika na kuanza kufanya kazi, mfumo huo utaimarisha zaidi ulinzi wa anga la Tanzania. 
  • Amesema kwa kiasi kikubwa rada hiyo pamoja na zile zitakazojengwa Mwanza, Songwe na Kilimanjaro zitasimamiwa na TCAA ikiwamo kuziongoza ili kuhakikisha ulinzi unaimarishwa zaidi.
  • Jiwe la msingi la ujenzi wa mfumo huo wa rada liliwekwa Aprili 2, 2018 na Rais John Magufuli na utagharimu Sh67 bilioni zikijumuisha mfumo wa rada uliojengwa katika viwanja vya ndege vya Mwanza, Kilimanjaro na Songwe.

 

 

 

 

 

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA ATEMBELEA RUKWA.. AANGAZIA AFYA, ELIMU, KILIMO NA MIUNDOMBINU KWA MIRADI YA MAENDELEO.

Katika ziara ya Rais Samia siku ya leo iliangazia kwenye sekta ya Afya, Elimu, Kilimo …

3 Maoni

  1. Rattling wonderful information can be found on blog.?

  2. Your style is unique in comparison to other people I’ve read stuff from. Thank you for posting when you have the opportunity, Guess I will just bookmark this blog.

  3. Very good write-up. I absolutely love this site. Thanks!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *