KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA CHAONGEZA UFANISI UTENDAJI KAZI ARDHI

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeboresha kituo chake cha Huduma kwa Wateja kwa lengo la kuwarahisishia wananchi kupata huduma za sekta ya ardhi kwa haraka na kwa ufanisi.

Kwa sasa kituo hicho kinahudumia idadi kubwa ya wateja wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani tofauti na hapo awali ambapo kwa sasa mara mteja anapofika Kituo cha Huduma kwa Wateja hupatiwa namba ya huduma inayomuwezesha kuhudumiwa kulingana na muda aliofika na eneo analohitaji kuhudumiwa.

Ad
Mkazi wa jiji la Dar es Salaam Charles Ndesanjo (kushoto) akipokea hati ya kiwanja chake kilichopo Bagamoyo mkoa wa Pwani kwenye Kituo cha Huduma kwa Wateja kilichopo Dar es Salaam.

‘’Unapofika kituo chetu cha Huduma kwa Wateja  pale umewekwa utaratibu maalum ambapo mteja anahudumiwa kwa wakati na taarifa zote zinazohusiana na ardhi zipo kwa kuwa kuna mfumo unganishi wenye taarifa za upimaji, mipango miji pamoja na hati na suala la  kutatua mgogoro ni rahisi zaidi’’ alisema Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dar es Salaam Idrisa Kayera.

Kwa mujibu wa Kayera, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeamua kuboresha kituo hicho ili kuwezesha huduma za sekta ya ardhi zitolewe kwa haraka na ufanisi kwa kuwa huduma zinazohusu mipango miji, upimaji, maandalizi ya hati pamoja na taarifa za kodi zinapatikana kwenye kituo hicho.

Kamishna huyo Msaidizi wa Ardhi aliyekuwa akizungumza jijini Dar es Salaam jana kuhusiana na kituo hicho, alisema Wizara yake imeweka pia maeneo ya kulipia kodi na tozo mbalimbali karibu na kituo hicho lengo likiwa kuhakikisha huduma inapatikana kwa haraka zaidi.

Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dar es Salaam Idrisa Kayera akisisitiza jambo alipokuwa akielezea uboreshaji huduma za sekta ya ardhi katika mkoa wake kupitia Kituo cha Huduma kwa Wateja.

 ‘’Mtu akija atakuta kuna benki karibu kwa ajili ya kufanya malipo na pia kumbukumbu zake za nyaraka kuhusiana na masuala ya ardhi atazikuta, ramani za eneo na picha ya anga ya mkoa wa Dar Es Salaam ipo, kwa hiyo tunaweza kutatua migogoro kwa urahisi na kushughulikia changamoto’’ alisema Kayera.

Kwa upande wake Msimamizi wa Kituo cha Huduma kwa Wateja Bi. Bayumu Mushi alisema uanzishwaji kituo hicho ulilenga kuondoa kero waliyokuwa wakiipata wananchi wanapofuata huduma za ardhi ambapo awali walipotaka huduma walimfuata afisa ardhi yeyote lakini sasa wanapofika eneo la mapokezi huulizwa shida na kupelekwa kwenye dawati husika.

Mmoja wa wateja waliofika kituo hicho cha Huduma kwa Wateja Charles Ndesanjo alisema ameridhishwa na huduma zinazotolewa na kituo hicho kwani aliweza kuhudumiwa haraka kupata hati yake ya ardhi katika kiwanja chake kilichopo Bagamoyo mkoa wa Pwani tofauti na matarajio yake.

Naye Mwakilishi wa Kampuni ya uwakili ya Idda Attorney Bi. Eliminata Membo alikielezea kituo hicho kama mkombozi kwao kwa kuwarahisishia sana kazi za kufuatilia nyaraka mbalimbali za ardhi kutoka kwa wateja.

Alex Riwa mkazi wa Airport mtaa wa Mogo jijini Dar es Salaam alielezea kituo hicho kuwa kimesaidia kwa asilimia 80 kushughulikia kero za wananchi na kuondoa urasimu uliokuwemo awali katika ofisi hiyo. Amezitaka ofisi nyingine za ardhi katika mikoa nchini kuiga mfano wa ofisi ya Dare es Salaam kwa kuanzisha kituo cha huduma kwa wateja ili kuondoa kero kwa wananchi wanaohitaji huduma za ardhi.

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS.DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MJADALA WA KIMATAIFA WA CHAKULA

Katika tukio maalum la Mjadala wa Kimataifa wa Chakula, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa …

209 Maoni

  1. Priyanka Chopra https://baywatch.priyankachopra-ar.com is an Indian actress, singer, film producer and model who has achieved global success.

  2. When Taylor Swift https://shake-it-off.taylor-swift-ar.com released “Shake It Off” in 2014, she had no idea how much the song would impact her life and music career.

  3. The Formula One World Championship https://world-circuit-racing-championship.formula-1-ar.com, known as the Formula Championship in motor racing, is the highest tier of professional motor racing.

  4. After some difficult years in the late 2010s, Manchester United https://england.manchester-united-ar.com returned to greatness in English football by 2024.

  5. Michael Jordan https://chicago-bulls.michael-jordan-ar.com is one of the greatest basketball players of all time, whose career with the Chicago Bulls is legendary.

  6. Mike Tyson https://american-boxer.mike-tyson-ar.com one of the most famous and influential boxers in history, was born on June 30, 1966 in Brooklyn, New York.

  7. Muhammad Ali https://american-boxer.muhammad-ali-ar.com is perhaps one of the most famous and greatest athletes in the history of boxing.

  8. The golf https://arabic.golfclub-ar.com industry in the Arab world is growing rapidly, attracting players from all over the world.

  9. The Italian football championship https://italian-championship.serie-a-ar.com known as Serie A, has seen an impressive revival in recent years.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *