Maktaba ya Mwezi: May 2021

TANZANIA NA KENYA ZAKUBALIANA KUONDOA VIKWAZO 30 VYA BIASHARA VISIVYO VYA KIUSHURU, VIKWAZO VINGINE 34 VIPO KWENYE MKAKATI WA UTEKELEZAJI

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (Mb) amewahamasisha  wafanyabiashara wa Kitanzania kuendelea kufanya biashara na kwenda kuwekeza nchini Kenya kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo iliyopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki  na amewataka  kuwasiliana na Wizara iwapo kutakuwa na changamoto zozote. Hayo ameyasema katika Mkutano wa tano (5) …

Soma zaidi »

MKUU WA MAJESHI YA ULINZI TANZANIA JENERALI VENANCE MABEYO ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA- PRETORIA

Na Mwandishi wetu, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo,ametembelea Ubalozi wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania nchini Afrika Kusini. Jenerali Mabeyo yupo Nchini Afrika Kusini kuhudhuria sherehe za kumuaga Mkuu Majeshi wa Afrika Kusini Jenerali SZ Shoki zilizofanyika kitaifa Jana Mjini Pretoria. Kuhudhuria sherehe hizi,ni utaratibu uliowekwa …

Soma zaidi »

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa baadhi ya Makatibu Tawala wa Mikoa, kuwahamisha baadhi na wengine kuwabakisha katika vituo vyao vya kazi. Pia amefanya uteuzi wa viongozi wakuu wa taasisi kama ifuatavyo; Makatibu Tawala wa Mikoa walioteuliwa. Amemteua Bw. Rodrick Mpogolo kuwa …

Soma zaidi »

MAWAZIRI SEKTA YA BIASHARA EAC WAKUBALIANA KUONDOA VIKWAZO VISIVYO VYA KIBIASHARA

Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) la Jumuiya ya Afrika Mashariki lakubaliana kuondoa vikwazo visivyo vya kibiashara na kuimarisha biashara na uwekezaji ndani ya Jumuiya hiyo. Awali akifungua mkutano Jijini Arusha jana Ijumaa, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya …

Soma zaidi »

WAZIRI MKUU MAJALIWA: MARA WEKENI MKAKATI WA KUITANGAZA MBUGA YA SERENGETI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa Mkoa wa Mara na Watendaji katika Sekta ya Utalii wabadilike na waweke mkakati wa kuitangaza mbuga ya Serengeti ili kuweza kuvutia zaidi watalii na kuitambulisha mbuga hiyo kuwa iko mkoa humo. Amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan …

Soma zaidi »

RAIS SAMIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA DKT. PHUMZILE MLAMBO MSAIDIZI WA KATIBU MKUU WA UN

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake UN Women Dkt. Phumzile Mlambo Ngcuka mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar …

Soma zaidi »

MAJALIWA AAGIZA UCHUNGUZI WATENDAJI WIZARA YA FEDHA

Waziri Mkuu, Mheshimwa Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Mkaguzi Mkuu,  Mkaguzi  Msaidizi pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha  za umma zinazowakabili. Akizungumza katika Kikao Kazi na Waziri wa Fedha na Mipango, Kaibu Mkuu,Manaibu  Katibu Wakuu na Watendaji Waandamizi wa Wizara …

Soma zaidi »