Waziri ya Madini, Mhe. Anthony Mavunde ameipongeza Bodi ya Wakurugezi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), kwa kulisimamia vema shirika hilo na kulifanya ling’are kwa kuwa moja ya mashirika ya umma yaliyopiga hatua kiasi cha kutoa gawio la Sh bilioni nane kwa Serikali.