SERIKALI YA TANZANIA YAFANYA MAZUNGUMZO NA MTAALAM WA UMOJA WA MATAIFA KUHUSU HAKI ZA WATU WENYE UALBINO

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amefanya mazungumzo na Mtaalam wa kujitegemea wa masuala ya haki za Watu wenye Ualbino kutoka Umoja wa Mataifa (UN Independent Expert on the Enjoyment of rights by Persons with Albinism), Bi. Muluka-Anne Miti-Drummond leo Februari 6, 2024, jijini Dodoma. 

Katika kikao hicho miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na Mpango Kazi wa Umoja wa Afrika kuhusu masuala ya Watu wenye Ualbino, Kujadili Rasimu ya Mpango Kazi wa Watu wenye Ualbino na hatua zilizochukuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu ujumuishwaji wa Watu wenye Ualbino na ufikiwaji wa huduma ya afya, haki zao na elimu jumuishi. 

Ad

Akizungumza kwenye kikao hicho, Waziri Ndalichako amebainisha kuwa, Serikali kwa kushirikiana na Chama cha Watu wenye Ualbino (TAS)pamoja na Wadau wa maendeleo wanaoshughulika na masuala ya Watu wenye Ualbino nchini wameandaa rasimu ya Mpango Kazi wa Taifa kwa Watu wenye Ualbino (MTAWWU, 2023/2024 – 2027/2028) ambao umejikita katika kutokomeza ubaguzi na ukatili dhidi ya watu wenye ualbino.

Vile vile, Prof. Ndalichako amesema Serikali ya Tanzania imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha usawa, haki, fursa, huduma bora na ustawi kwa watu wenye ulemavu ikiwamo huduma ya afya, haki ya elimu, ajira, miundombinu rafiki na upatikanaji wa vifaa saidizi.

#NA HAYA NDIYO MATOKEO CHANYA+

Ad

Unaweza kuangalia pia

Je! Wajua Mchango wa Madini ya Tanzanite katika Pato la Taifa?

Madini ya Tanzanite, yanayopatikana pekee katika eneo dogo la Mererani, Tanzania, ni miongoni mwa rasilimali …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *