Recent Posts

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Rais wa Sierra Leone Mhe. Julius Maada Bio kushoto pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina

Hii ni mara baada ya kushiriki Mjadala wa Kimataifa wa Norman E. Borlaung wenye lengo la kutafuta suluhu ya changamoto ya upatikanaji wa chakula Duniani inayochochewa na mabadiliko ya tabianchi. Mjadala huo umefanyika katika Mji wa Des Moines, Iowa nchini Marekani tarehe 31 Oktoba, 2024. #NaHayaNdiyoMatokeoChanyA+ #MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM …

Soma zaidi »

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya majadiliano (round tables discussion) na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo ikiwemo Viongozi wa Serikali ya Marekani, wamiliki wa makampuni binafsipamoja na Taasisi zisizo za Kiserikali (NGOs) leo tarehe 31 Oktoba 2024, mjini Iowa, Marekani

Mazungumzo hayo yalijikita katika kujadili fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta ya kilimo zinazopatikana Tanzania na namna Tanzania inavyoweza kunufaika kupitia wawekezaji hao. #MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya #Kilimo

Soma zaidi »

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye mjadala (round tables discussion) kuhusu Kilimo barani Afrika, katika Mji wa Des Moines, Iowa nchini Marekani tarehe 30 Oktoba, 2024

Mjadala huo ambao uliandaliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka barani Afrika, Serikali na Sekta binafsi ya Marekani hususan waliopo kwenye sekta ya kilimo. #MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya #Kilimo

Soma zaidi »