Maktaba Kiungo: UMEME VIJIJINI

DKT. KALEMANI AITAKA TANESCO KUENDELEZA MIRADI YA UMEME VIJIJINI

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuendelea kusambaza umeme vijijini mara wakandarasi wa umeme vijijini wanapomaliza kazi kwa mujibu wa mkataba. Dkt. Kalemani aliyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kukagua kazi ya usambazaji umeme vijijini katika Wilaya za Mpwapwa na Bahi mkoani Dodoma ambapo aliambatana …

Soma zaidi »

IFIKAPO JUNI 30,MITAA YOTE YA MAJIJI IWE IMESAMBAZIWA UMEME – DKT. KALEMANI

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amewaagiza watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha kuwa ifikapo tarehe 30 Juni, 2019, mitaa yote isiyo na umeme katika Majiji yote nchini iwe imesambaziwa umeme. Dkt Kalemani aliyasema hayo tarehe 5 Mei, 2019, mara baada ya kufanya ziara katika maeneo mbalimbali jijini …

Soma zaidi »

UWEKEZAJI KWENYE MIRADI YA UMEME VIJIJINI UCHAGIZE UKUAJI WA UCHUMI – SIMBACHAWENE

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, George Simbachawene ametoa wito kwa Serikali kuhakikisha kuwa uwekezaji mkubwa unaofanywa katika miradi ya umeme vijijini unachagiza ukuaji wa uchumi kwa kupeleka umeme unaotosholeza mahitaji ya wananchi na kusambaza umeme katika Taasisi za Serikali na kijamii. Simbachawene ameyasema hayo jijini Dodoma, …

Soma zaidi »

MRADI WA UMEME WA KINYEREZI 1 EXTENSION KUKAMILIKA MWEZI AGOSTI 2019

Imeelezwa kuwa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi wa Kinyerezi I extension utakamilika mwezi Agosti mwaka huu ambapo utazalisha umeme wa kiasi cha megawati 185. Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam tarehe 28 Aprili, 2019 na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa miradi …

Soma zaidi »

WAZIRI WA NISHATI AKUTANA NA WAKANDARASI MIRADI YA UMEME VIJIJINI GEITA

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amekutana na wakandarasi wa miradi ya umeme vijijini katika Mkoa wa Geita na kujadiliana kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo kwa ufanisi zaidi. Katika kikao hicho kilichofanyika, Aprili 20, 2019 katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Chato, makubaliano maalum yaliyofikiwa ni kwa wakandarasi husika …

Soma zaidi »

HAKUNA SIKUKUU KWENYE KAZI ZA UMEME – WAZIRI KALEMANI

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amewaagiza amewaagiza wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini kuendelea na kazi katika maeneo yao kwa siku zote zikiwemo sikukuu. Alitoa maagizo hayo Aprili 18, 2019 Kongwa, Dodoma alipokuwa akikagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini; ambapo pia aliwasha umeme katika vijiji vya Ngonga na …

Soma zaidi »

WAZIRI KALEMANI ASISITIZA TAASISI ZA UMMA VIJIJINI ZIWEKEWE UMEME

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amewaagiza wataalamu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuwasimamia wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini nchi nzima, kuhakikisha wanatoa kipaumbele cha kuunganisha umeme kwa taasisi zote za umma zilizo katika maeneo yao. Alitoa maagizo hayo kwa nyakati tofauti jana, Aprili 16, 2019 akiwa katika …

Soma zaidi »

SERIKALI YATENGA FEDHA ZA NDANI KUPELEKA UMEME WA GRIDI KATAVI

Imeelezwa kuwa, Serikali imetenga fedha za ndani, kiasi cha Dola za Marekani milioni 70 kwa ajili ya kazi ya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kV 132 kutoka Tabora hadi Katavi ambayo itawezesha Mkoa wa Katavi kuunganishwa na gridi ya Taifa. Hayo yalisemwa na Waziri wa Nishati, …

Soma zaidi »