RAIS SAMIA AZUNGUMZA KWA NJIA YA MTANDAO NA BW. BEN VAN BEURDEN AFISA MTENDAJI MKUU WA KAMPUNI YA ROYAL DUTCH SHELL

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 04 Oktoba, 2021 amezungumza kwa njia ya mtandao na Bw. Ben Van Beurden Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Royal Dutch Shell yenye makao yake makuu  nchini Uholanzi.

Bw. Van Beurden amemshukuru Mhe. Rais Samia na kueleza kuwa wanaridhishwa na jinsi Serikali ya Awamu ya Sita ilivyoboresha mazungumzo ya uwekezaji  kwenye mradi wa Gesi asili iliyosindikwa (LNG) hapa nchini.

Ad

Kwa upande wake Rais Samia amemshukuru Bw. Van Beurden kwa nia yao njema ya kutaka kuwekeza kwenye mradi huo ambao utachochea kukuza uchumi wa Tanzania.

Kikao hicho kilichofanyika kwa njia ya mtandao Ikulu Chamwino mkoani Dodoma,  kimehudhuriwa na Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi. Leonard Masanja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dkt. James Mataragio.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba amekutana kwa mazungumzo na Waziri wa Biashara, Uchumi, Nchi zinazozungumza Kifaransa na Wafaransa waishio nje ya nchi, Mhe. Frank Reister katika ofisi za Wizara jijini Paris, Ufaransa tarehe 15 Mei, 2024.

Mawaziri hao wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha ushirikiano kwenye masuala ya biashara na uwekezaji …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *