Nukuu za Rais Dkt. John Magufuli katika Kikao kilichowakutanisha viongozi Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Wakuu wa Mikoa, Mawaziri na Makatibu Wakuu wa baadhi ya Wizara.
- “Na saa nyingine huwa ni vigumu ukishasifiwa maeneo mengine yote halafu ukakuta eneo unalolisimamia usisifiwe, huwa linavunja moyo. Lakini ni vyema niwaeleze ukweli na nitatoa takwimu nikilinganisha na nchi nyingine”:-
- “Ukilinganisha labda na nchi zilizoko ndani ya Afrika.. nchi ya Tanzania yenye idadi ya watu karibu milioni 54-55, idadi ya walipa kodi ukiacha hizi juhudi ambazo zimezungumzwa sasa, ilikuwa ni watu 2,273,153! 2,273,153… katika nchi yenye idadi ya watu milioni karibu mil. 54-55! Uwiano wa kodi wa GDP kwa % tuna 12.8;
- Ukienda Kenya, ina idadi ya watu mil 46,600,000 idadi ya walipa kodi ni 3,940,000. Uwiano wa kodi kwa GDP kwa % ni 18.5%. Sisi tuko 12.8% ; Kenya ambao ni wachache zaidi.. sisi tuko mil 55 wao mil. 46, wako 18.5%! Rwanda; Idadi ya watu Rwanda ni 11,671,371. Walipakodi ni 172,422. Uwiano wa kodi kwa GDP ni 15.8%. Uganda; Idadi ya watu 37,746,217. Walipakodi ni 1,320,621. Uwiano wa kodi kwa GDP ni 14.2%.
- Burundi; Idadi ya wananchi wa Burundi ni 10,400,938. Idadi ya walipa kodi 22,591. Uwiano kwa kodi kwa GDP ni 13%. Afrika ya Kusini; Idadi ya wananchi ni 56,522,000. Walipakodi wao ni 19,980,110. Uwiano wa kodi kwa GDP ni 26%. Sisi 12.8%.. Afrika ya kusini ambayo idadi ya population Inakaribiana karibiana, wao ni 26%! Botswana; Idadi ya watu wa nchi ya Botswana ni 2,254,021. Walipakodi wao ni 734,470. Uwiano wa kodi kwa GDP ni 14%. Zambia; Wako 16,405,229. Walipakodi ni 872,748. Uwiano wa kodi kwa GDP 15.8%. Msumbiji; Wako 27,128,530. Walioakodi wa Msumbiji ni 5,321,669!. Wako mil.27.1, walipakodi ni mil.5.3! Uwiano wa kodi kwa GDP ni 18%.
- Namibia; Wako milioni 2.3 Walioakodi wao ni 666,763! Ni almost moja ya Tatu ya Wanamibia wanalipa kodi! Uwiano uko 12%Unapoangalia takwimu hii, ndipo sisi wakusanya Kodi na Wizara ya fedha ndipo mahali panapotakiwa kuanza kujiuliza!..”- Rais Dkt. John Magufuli. Dec 10,2018
Ad