RAIS MAGUFULI AKAGUA MAANDALIZI YA SHEREHE ZA UWEKAJI JIWE LA MSINGI UJENZI WA OFISI ZA IKULU CHAMWINO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi za Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi za Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma

Rais Dkt. John Magufuli amekagua maandalizi ya sherehe za uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi za Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma zitakazofanyika kesho tarehe 30 Mei, 2020.

Jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi hizo litawekwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Mama Maria Nyerere (kwa niaba ya Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere), Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Dkt. Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Ad

Sherehe hizo zinatarajiwa kuanza saa 3:00 asubuhi na zitarushwa moja kwa moja na vyombo vya habari vya redio, televisheni na mitandao.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi za Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi za Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma
Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: RAIS MAGUFULI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA (LAW DAY ) – JNICC DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 06 Febuari, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.